fbpx

Instagram Waleta ‘Instagram Direct’; Onesha Picha Kwa Chaguo Lako

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Instagram wameleta kitu kizuri zaidi katika kukupa uhuru wa kuamua nani aone picha unayoweka katika mtandao huo. Hii ni pamoja na mtu mmoja, au kundi la watu fulani.

Habari hii imetangazwa ramsi leo hii na katika baadhi ya nchi kama Marekani tayari watu wameweza kutumia uwezo huo mpya kupitia toleo jipya (update) ya Instagram iliyotolewa leo hii. Hadi mara ya mwisho nimeangalia katika Google Play ilikuwa bado haijaingizwa, hivyo tutegemee masaa yeyote kuanzia sasa. Kwa sasa uwezo huo utakuwepo kwa matoleo ya Instagram ya Androd, na iOS. Watumiaji wa simu za Windows itawabidi kusubiri kidogo.

Je unadhani kuna umuhimu sana wa uwezo huu?

MABADILIKO(7:31 Usiku): Tayari Instagram Direct inapatikana kwa iOS (iPhones na iPads) Tanzania.
Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  HUAWEI ASCEND P6: Huawei Waitambulisha Simu Nyembamba Zaidi!
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply