Kuna taarifa kuwa mtandao wa kijamii unaokuwa kwa kasi zaidi wa Instagram kuwekewa uwezo wa kuweza kutumiana ujumbe wa maneno, ‘Chat’ katika toleo linalokuja (update).
Instagram ni mtandao wa kijamii unaowawezesha watumiaji kupiga picha au kurekodi video fupi na kisha kuweza kubadili mtazamo wa kirangi wa picha/video hizo (effects).
Inasemekana kuwa uwezo wa ‘chat’ utakuwa wa watu wawili na pia zaidi ya wawili maarufu kwa lugha ya bibi Elizabeth kama ‘Group Chat’. Kwa sasa watumiaji wa Instagram wanaweza kuchati kwa kutumia apps nyingine zinazowaunganisha marafiki wa Instagram kama vile InstaMessage (Kushusha bofya Android au iOS).
Uwezo huu wa chati unategemewa kuwezeshwa ndani ya mwezi wa kumi na mbili. Je utafurahia uwezo huo au unaona hakuna umuhimu wa kuwa na chati katika Instagram?
No Comment! Be the first one.