Unapokua namba 3 katika simu na bado huna App ya picha maarufu zaidi, Instagram, wateja lazima wakufikirie vingine tofauti na simu za Apple na Android . Lakini hiyo imeshabadilika instagram imeingizwa rasmi katika market ya simu za windows hivyo watumiaji wote wanaweza download na
kuanza ku ‘share’ picha mbalimbali . Licha ya hvyo bado kuna wigo mpana kwa sababu windows phone wana app 190,000 wakati Apple na Android zinafika takribani milioni. Hata hivyo Windows wanaweza sema wana App nyingi ambazo ni nzuri kwa sasa japokua hawazidi hao wapinzani wao wawili. Instagram inaungana na App zingine ambazo hazina mda sana tangia ziingizwe katika windows ambazo ni Vine, App maarufu ya video, social magazine Flipboard, game ya Temple Run 2, TuneIn Radio na Line mtandao wa kijamii ambao umejikita sana Japan. Katika App 10 zilizokua zinadownloadiwa sana Apple sasa zote zipo katika windows (hizo ni Facebook, Pandora, Skype, Words with Friends, The Weather Channel, Twitter, YouTube, Google Search , Instagram na Temple Run). Risecha wa masoko ‘ Canalys’ amesema kuwa kati ya App 50 za bure zilizopo Apple App Store na Googleplay Store, 30% tuu ndio zilikua zinaonekana katika Windows mwezi wa tano. Japokua wigo unapungua lakini bado kuna App nzuri bado hazipo windows mfano game ya ;candy crush saga’ hata soundcloud na App zingine
kuteka akili za wateja Microsoft na wazalishaji wa simu za Nokia wanajitahidi kutoa simu ambazo zina mambo bora na ya hali ya juu ambayo hayapatikani katika simu zingine kwa mfano Nokia Lumia 1020 ina kamera yenye 41-megapixel na bado ina screen kubwa kuliko Apple wala Android
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Mbunifu na mpenda teknolojia.
Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM
Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.
| mhariri(at)teknokona.co.tz |
No Comment! Be the first one.