Kampuni ya Apple Inc. imeripotiwa rasmi kuwa wamiliki wa kampuni ya ‘headphone’ ya Beats Electronics baada ya kutumia takribani dola bilioni tatu za kimarekani kuinunua kampuni hiyo iliyoanzishwa na prodyuza mkongwe wa miondoko ya hiphop, Dr. Dre na mwenzake Jimmy Lorine wa Interscope records.
Kampuni hiyo ambayo pia inatoa huduma ya kusikiliza muziki mtandaoni imeifanya Apple kutumia hela nyingi zaidi ya manunuzi yote iliyowahi kufanya.
Katika dili hilo lililofanyika rasmi baada ya wiki kadhaa za hayawi hayawi, inasemekana Dr. Dre na Jimmy Lorine watabaki kwenye kampuni hiyo ‘iliyokuwa’ wakiwa waajiriwa wa kampuni ya Apple ingawa haijajulikana watakuwa na vyeo gani.
No Comment! Be the first one.