Moja ya sekta ambayo nchi nyingi duniani zinaingiza pato kubwa ni kwenye sekta ya mawasiliano ambayo katika maisha yetu ya kila siku kuna mambo mengi lazima yahusishe sekta hii, inaweza ikawa kwa mawasiliano ya simu, barua pepe, n.k.
Kama nchi kupitia mamlaka husika mathalani Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatakiwa kuwa na mfumo imara wa kusimamia mawasiliano ya simu ambapo hakuna sekunde inapita bila ya watu kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi, barua pepe.
Toka mwaka 2013 Tanzania iliamua kuwa na Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS-Telecommunications Traffic Monitoring System) ambao kazi yake ni:-
Kuwa na rekodi ya mawasiliano ya simu (traffic); Simu zinapigwa kutoka wapi, kwenda wapi na kwa mazungumzo ya muda gani.
Kutambua mapato na takwimu za miamala ya fedha mitandaoni pamoja taarifa za kadi ya simu na namba tambulishi za kifaa cha mawasiliano.
Kuwa na uwezo wa kugundua utapeli wa aina yoyote unaohusisha mitandao ya simu au mtu yeyote mwingine mwenye uwezo wa kufanya udanganyifu wa kimawasiliano; mfano uwezo wa kupiga simu bure, n.k.
Vilevile, kusimamia kwa ufanisi ubora wa huduma za mawasiliano ili kuboresha viwango vya huduma hizo.
Hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu uliokabidhiwa TCRA.
Ujio wa mfumo huo ulichagizwa na ripoti ya mwaka 2014-15 kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali iliyobainisha upotevu wa Tsh. bilioni 400 kwa TCRA kutoka kenye makampuni ya simu.
Kabla ya hapo TCRA ilikuwa ikipata bilioni 42 pekee kutokana mtambo ambao kampuni ya Uswizi inaumiliki kutokana na mkataba waliokuwa wameingia na mamlaka husika kufanya kazi ambayo mfumo wa sasa inafanya.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|