fbpx

Kompyuta, Laptop, Teknolojia

Mauzo ya Kompyuta 2020 yapo juu, Laptop za Chromebooks nazo juu

mauzo-ya-kompyuta-2020-chromebooks

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Mauzo ya kompyuta 2020 yapo juu,  Data za kimauzo kutoka shirika la tafiti za masoko la Canalys zinaonesha kuna jumla ya kompyuta milioni 79 ziliuzwa katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka huu (Julai – Septemba 2020).

Janga la COVID19 – Korona lililosababisha watu wengi wafanyie kazi majumbani limechangia katika ukuaji huu wa mauzo wa kompyuta. Na mauzo haya yanaonekana ni habari njema kwa kompyuta zinazotumia programu endeshaji ya Chrome OS, zinazofahamika kwa jina la Chromebooks.

Mauzo ya kompyuta milioni 79 ni ukuaji wa asilimia 12.7 ukilinganisha na mauzo ya kipindi kama hicho mwaka jana, yaani Julai hadi Septemba 2019.

Katika mauzo hayo vifaa vya kompyuta kwenye makundi ya ‘notebooks’, yaani laptop pamoja na tableti ndizo zilizouzika zaidi. Hizi zilichangia mauzo ya milioni 64 kutoka kwenye ile jumla ya vifaa milioni 79 vilivyouzwa. Idadi inayobaki ambayo ni asilimia 28.3 ni ya uuzaji wa kompyuta kubwa – za mezani.

mauzo ya kompyuta 2020Makampuni yanayoongoza kimauzo: Lenovo, HP na Dell wanaoshikilia nafasi tatu za juu kimauzo – ndio wote kwa pamoja wameuza asilimia 65.4 ya hizo kompyuta milioni 79.

Lenovo anashikilia nafasi ya kwanza kwa kuuza vifaa milioni 19, HP nafasi ya pili kwa kuuza kompyuta milioni 18.6 na huku Dell akiuza kompyuta milioni 11.9. Lenovo na HP wote wana ukuaji wa mauzo wa zaidi ya asimilia 10 kila mmoja ukilinganisha na mauzo ya mwaka jana, huku Dell mauzo yakiporomoka kwa asilimia 0.5.

SOMA PIA  FACEBOOK: Dondosha Comment Hata Kama Huna Intaneti!

Kompyuta za Familia ya Chromebooks.

chromebook
Laptop ya Chromebook kutoka Lenovo

Chrome OS ni programu endeshaji ya kisasa inayotengenezwa na Google. Tayari makampuni mengi kama hayo niliyoyataja hapo juu yanatengeneza laptop zinazokuja na programu endeshaji ya ChromeOS. Bila kujali watengenezaji wa laptop husika, laptop zinazotumia programu endeshaji ya ChromeOS huwa zinapewa jina la Chromebook.

Soma Pia -> Apps za Android zaanza kutumika katika Laptop za Chrome OS

Laptop za familia ya Chromebook nazo zinaendelea kuonesha ukuaji wa kasi katika mauzo yake. Kwa ujumla Chromebooks milioni 9.4 ziliuzwa katika kipindi cha Julai – Septemba mwaka huu, huu ukiwa ni ukuaji wa mauzo wa asilimia 122 ukilinganisha na mauzo ya mwaka jana kipindi kama hicho. Katika kipindi hicho cha miezi mitatu HP aliuza Chromebooks milioni 3.2, huku Lenovo naye akiuza laptop za Chromebooks milioni 1.8 – kwa Lenovo idadi hiyo ni ukuaji wa asilimia 300 ukilinganisha na mauzo yao ya Chromebooks katika kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

SOMA PIA  Google Translate Sasa Inahushisha Lugha 103!

Je unatumia kompyuta gani kwa sasa? Je huwa unaaangalia nini pale unapotaka kununua laptop mpya? Soma makala yetu ya Mambo 4 Muhimu ya Kufahamu katika Ununuaji wa Laptop

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |

Toa Maoni

Your email address will not be published. Required fields are marked*