Google ni moja kati ya makampuni makubwa sana katika nyanya ya teknolojia na kwa sasa wanatamba sana na simu zao za Google Pixel lakini kwa sasa wanaingia kabisa katika soko la simu janja za kujikunja na wanakuja na Google Pixel Fold.
Licha ya kuwa soko la simu za kujikunja kwa sasa limetawaliwa na kampuni ya Samsung—maana wao ndio wanafanya vizuri zaidi—katika soko. Kumbuka tuliandikia kuhusiana na Google Pixel Fold kwa mara ya kwanza kabisa >>HAPA<<
Mpaka sasa kampuni bado haijato sifa hata moja ya undani kuhusiana na simu janja hiyo lakini ni kinachofahamika dhahiri ni kwamba wiki ijayo kila kitu kitafahamika sababu kutakua na tukio la uzinduzi wa simu hii.
Kile ambacho kampuni imefanya ni kutoa video fupi ikiwa inaonyesha jinsi simu hiyo ilivyo –kimuonekano, aina yake ya kamera zake haina tofauti kubwa kimuonekano ukilinganisha na simu janja zake za Pixel.
Kwa mujibu wa fununu ni kwamba simu janja hiyo ya kujikunja itakua na kioo cha inchi 5.8 hapo ukiwa hujaikunjua na ukifanikiwa kuikunjua itakwenda na mpaka kioo cha inchi 7.6
Simu hii iliku inategemewa kuingia katika soko mwaka jana lakini wengi walishaanga katika tamasha la I/O la 2022 la Google hii haikutangazwa lakini katika I/O la mwaka 2023 uhakika upo.
Kingine ambacho google wamekua wakitilia mkazo sana ni katika kuhakikisha kuwa wanawapa elimu ya kutosha waandaaji wa App (developers) katika kuhakikisha App zao zitakua zinafanya kazi vizuri kabisa katika
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani Pixel fold ndio atakua mshindani mkuu katika soko la simu janja za kujikunja au Samsung bado ataendelea kuburuza?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
No Comment! Be the first one.