fbpx

Kompyuta, Laptop, Lenovo, Teknolojia, Uchambuzi

ThinkPad X1 Fold: Lenovo waja na laptop yenye skrini inayokunjika

thinkpad-x1-fold-lenovo-laptop-skrini-inayokunjika

Sambaza

Lenovo wametambulisha laptop mpya inayokwenda kwa jina la ThinkPad X1 Fold laptop yenye skrini yenye uwezo wa kukunjwa.

Laptop hii inayotumia programu endeshaji ya Windows 10, inachukua sifa ya kuwa laptop ya kwanza kuja na teknolojia hii ambayo tayari imeanza kuja kwenye simu – kama vile Samsung Galaxy Fold.ThinkPad X1 Fold laptop

SOMA PIA  Airtel Tanzania yapunguza gharama za mawasiliano

Laptop hii inaweza kutumika kama tableti lakini pia inaweza kutumika kama kompyuta kamili kutokana na uwezo wa kutumia keyboard za mfumo wa bluetooth. Inaukubwa wa inchi 13.

 

ThinkPad X1 Fold
Inakuja na keyboard inayotumia bluetooth pamoja na uwezo wa kutumia peni kwenye skirini (Stylus).

Sifa na uwezo wake

  • Inakuja prosesa ya Intel Lakefield
  • Port mbili za USB-C
  • Uwezo wa kutumia laini (Sim Card)
  • Uwezo wa RAM wa GB 8
  • Uwezo wa Diski Uhifadhi wa TB 1
  • Uzito wa takribani kilogramu 1.1
  • Teknlojia ya 5G
SOMA PIA  Pata Taarifa za Simu Yako ya Android/ iPhone bila Kuigusa

Laptop ya ThinkPad X1 Fold imeanza kupatikana kwa malipo ya awali (preorder) ya dola 2,499 (Zaidi ya Tsh Milioni 5 za kitanzania).

Vyanzo: The Verge, Lenovo na tovuti mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |

Toa Maoni

Your email address will not be published. Required fields are marked*