Ubia wa Blackberry na Emtek. Katika kujaribu kuongeneza mapato Blackberry wameingia ubia na kampuni ijulikanayo kama ‘Emtek’ kutoka nchini Indonesia kusaidia BBM app irudishe makali yake kama ilivyokuwa zamani.
Elang Mahkota Teknologi(Emtek) inamiliki televisheni 2 za taifa, tovuti za kuweza kupata habari online na nyumba za kufanyia maigizo, n.k. Kitendo cha Emtek kuingia ubia na Blackberry kitawezesha Emtek kuweza kutangaza biashara zao katika BBM app na hivyo kupanua wigo wa biashara kwa makampuni hayo.
Ubia huo kati ya Emtek na Blackberry utawawezesha watumiaji wa app hiyo kuweza kupata matangazo mbalimbali, muziki video, games, n.k. Imeelezwa kuwa ubia huo kati ambao utadumu kwa zaidi ya miaka sita utawezesha Blackberry kulipwa jumla ya dola milioni 207(zaidi ya Tsh 455bn).
Nchini Indonesia BBM app inawatumiaji takribani milioni 60 kwa kila mwezi na ndio nchi pekee yenye watuaji hai(active) duniani kote na kwa jumla BBM app ina watumiaji ‘hai’ takribani milioni 90 kila mwezi. Emtek na KMK Online watarajia kufungua ofisi Toronto-Canada ili kuweza kufanya kazi karibu na Blackberry yenye makao makuu yake nchini Canada.
Emtek imekuwa ikifanya jitihada mbalimballi ili kujiongezea mapato yake na hayo yanajidhihirisha kwa kampuni hiyo kuwekeza zaidi kwenye biashara ya ku-stream online ambapo mapema mwaka huu Emtek walianzisha iFlix ambayo ni maalum kwa ajili ya kustream video online mchini Malaysia na baadae kuzinduliwa nchini Indinesia ili nao waweze kustream video online.
Je, unadhani ubia kati ya Emtek na Blackberry utaziwezesha kampuni hizo kujihimarisha na kuongeza mapato? Tuambie mani yako katika hili katika comment hapo chini. Endelea kuhabarika kupitia TeknoKona.
Vyanzo: Nikkei Asian Review, mobile world live