fbpx
Intaneti

PayPal ni nini? Ifahamu njia salama ya malipo ya kwa njia ya mtandao

paypal-ni-nini-njia-salama-ya-malipo-njia-ya-mtandao
Sambaza

PayPal ni kampuni ya nchini Marekani inayotoa huduma ya malipo kwa wauzaji na wananunuaji wa bidhaa kwa njia za mtandaoni. Nje ya malipo ya kibiashara, PayPal pia inatoa huduma ya malipo/kutumiana pesa kwa watu binafsi.

Paypal ni nini
Kupitia huduma ya PayPal, watu wanaopenda kufanya manunuzi na malipo ya huduma mbalimbali kwa njia za kimtandao wanakuwa salama zaidi.

Malipo yanaweza kutumwa kutoka kwa mtumiaji mmoja kwenda mwingine kwa njia mbalimbali kama vile;

  • Kwa kutumia anuani ya barua pepe ya mtumiaji mwingine au namba ya simu.
  • Kwa malipo ya huduma au bidhaa ukienda kwenye tovuti unayolipia au kununua kitu basi ukibofya sehemu ya ‘Pay with PayPal’, yaani lipa kwa PayPal utapelekwa kwenye tovuti ya PayPal na kisha utaruhusu malipo hayo kufanyika.
INAYOHUSIANA  Netflix Kuwa Juu Zaidi Wakati Amazon Na Disney+ Wakifukuzia!

Je, kuna faida gani za kutumia huduma ya PayPal?

Kwa nini utumie PayPal?

> Usiri na usalama wa data za kadi yako ya benki

Utakapojiandikisha katika mtandao wa PayPal utajaza taarifa za kadi yako ya Visa au MasterCard pamoja na taarifa nyinginezo za akaunti yako ya benki. Taarifa hizi zitahifadhiwa katika mfumo salama wa PayPal. Baada ya hapo utaweza kufanya malipo mbalimbali katika mitandao mbalimbali bila ya mitandao/makampuni hayo mengine kupewa taarifa zako za kibenki.

PayPal ndio atakuwa anawalipa hao wengine, na yote haya yanafanyika bila hao wengine kupata taarifa zako zozote muhimu za kadi yako ya benki.

> Utumaji wa Pesa

INAYOHUSIANA  Uhalifu wa mitandaoni unazidi kudhibitiwa

Huduma ya PayPal ya inaruhusu watu kuweza kutuma na kupokea pesa kutoka kwa watumiaji wengine. Ila kwa nchini bado huduma hiyo hairuhusu upokeaji wa pesa kwa watumiaji wa kawaida wa nchini Tanzania, na hata kwenye baadhi ya nchi nyingine nyingi – ni suala la kisheria na utaratibu itahitaji PayPal wafuate utaratibu wa kujiandikisha kwenye vyombo kama vile Benki Kuu (BOT) na vyombo vingine vinavyoratibu huduma za fedha.

Kwa hapa nchini mtumiaji anaweza kutuma pesa kwenda kwa watumiaji wengine walio katika nchi ambazo watumiaji wake wana uwezo wa kupokea pia – kama Marekani.

INAYOHUSIANA  Ifahamu 'Kiddle' Google Kwa Ajili Ya Watoto!
PayPal ni nini
Huduma za kutuma na kupokea pesa kwa watumiaji wa nchini Marekani zinakubalika kwa watumiaji wa kadi za aina mbalimbali za malipo ya benki; kama vile Visa, MasterCard na nyinginezo kama zinavyoonekana
PayPal ni nini
Huduma ya malipo na utumaji pesa kwa watumiaji wa Tanzania

 

> Hakuna makato ya kutumia huduma

Hakuna malipo ya mwezi au ya kujiandikisha na huduma hii. Ni bure. Hakuna makato utakayokatwa nje ya bei ya huduma au bidhaa unayonunua – anayekuuzia ndio anabeba malipo ya gharama za kukamilisha muhamala.

Jiunge na PayPal kwa kutembelea tovuti yao – www.paypal.com 

Haya ni machache kuhusu huduma ya malipo ya mtandaoni ya PayPal. Je, wewe ni mtumiaji wa huduma za PayPal? Una nini la kuwashauri/kuwaambia wengine kuhusu huduma hii?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |