fbpx
Kamera, simu, Teknolojia

Mwanamuziki John Legend atoa video mpya ya nyimbo iliyopigwa na Simu

john-legend-atoa-video-nyimbo-iliyopigwa-na-simu
Sambaza

Wakati simu janja zikiendelea kurahisisha maisha na kuongeza teknolojia ya juu zaidi, Mwanamuzi John Roger Stephens, maarufu kama John Legend ametoa video ya nyimbo yake mpya ya ‘Good Night’ aliyomshirikisha BloodPop kwa kutumia simu kupiga picha za video.

Kwa mara ya kwanza imetumika simu ya rununu kuchukua picha za video za nyimbo hiyo yote. Simu iliyotumika kuchukua video ni ya Google pixel 2.

INAYOHUSIANA  Waliopewa dhamana ya kusimamia mifumo ya TEHAMA serikalini waonywa na kutakiwa kuzingatia weledi kazini
nyimbo iliyopigwa na simu
Mwanamuziki John Legend

Katika mahojiano John Legend ameeleza sababu ya kutumia Google Pixel 2 ni kuwa aliona itakuwa nzuri kwani kamera ya Google Pixel 2 ni ya ajabu na inavutia sana. Aidha pia alisema inapunguza bajeti ya kutumia kamera kubwa.

Pia amesema amekuwa akiitumia google Pixel 2 katika kuchukua matukio mbalimbali ya familia yake na kuona uzuri na ubora wa picha za video kutoka katika simu hiyo.

INAYOHUSIANA  Hatimaye bajaji yenye kutumia nishati ya Jua yawasili Uingereza

Katika nyimbo hiyo ya Good Night inayoelezea mapenzi ambapo usiku mmoja unaweza kubadilisha maisha yako milele picha zote za Video kwa asilimia 100 zilichukuliwa na Google Pixel 2.

nyimbo iliyopigwa na simu
Uchukuaji picha za Video ukiendelewa kwa kutumia simu ya Google Pixel 2.

Simu ya Google Pixel 2 ilizinduliwa Oktoba mwaka 2017 ikiwa na ukubwa wa kioo cha inchi 5.0. Kwa upande wa kamera ina 12.2 MP (f/1.8, 27mm, 1/2.6″, 1.4 µm, Dual Pixel PDAF), OIS, phase detection & laser autofocus, dual-LED flash.

INAYOHUSIANA  Apple kuja na simu rununu zenye uwezo wa kukunja na kukunjua

Na kwa upande wa uchukuaji wa ubora wa Video ni 2160p@30fps, 1080p@30/60/120fps, 720p@240fps. Ni wakati wa wasanii wa Tanzania kuanza kupiga picha za video kwa kutumia simu zao ili kupunguza bajeti kubwa kwa kukodisha kamera.

Nyimbo hiyo ya Good Night ya John Legend waweza kuiangalia hapo chini.

Youtube

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.