WhatsApp haihitaji utambulisho kabisa na ni App ya kutuma na kupokea ujumbe inayopendwa sana na watu katika simu-janja za Android, iOs na Windows hata katika Blackberry. Mazungumzo mengi hufanyika Whatsapp ambapo kuna zaidi ya watumiaji milioni 500. Unaweza tuma picha, video na hata pia ujumbe wa sauti, lakini vipi ukitaka kutuma muziki? usifikirie sana Teknokona inakupa njia ni hapa
- PAKIA MUZIKI WAKO KATIKA GOOGLE DRIVE
Kwanza kabisa inabidi u upakie (upload) mziki unnaotaka au miziki unayotaka kuutuma katika google drive. Ili Kupakia bonyeza hapa, Google drive ikishafunguka jiandikishe au kama una akaunti yoyote ya google log in.
Ukisha Log in unaweza uka pakia miziki yako hapo kwa kubonyeza kialama cha kupakia kilichopo mkono wa kushoto juu kama inavyoonyeshwa
Chagua faili unalotaka kutuma kisa bonyeza fungua (open). mara baada ya kubonyeza fungua mafaili hayo yataanza kujipakia katika google drive kutoka katika hifadhi yako ya kawaida (local Storage)
Ukishamaliza ku pakia mafaili yako kwenye google drive funga kiboksi ambacho kilitokea wakati unaanza kupakia. Hapo utakuwa umeweka mafaili yako katika Google Drive. Uzuri wa hii ni kwamba unaweza ukayatazama mafaili hayo muda wowote na kwa kifaa chochote (simu aua Kompyuta). Pia unaweza kuyatuma kwa mtu yeyote unaetaka.
- PAKUA GOOGLE DRIVE KWA iOs
Ukishamalizana na hapo juu basi pakua (download) Google Drive kwenye simu yako ya iOs. Ukisha shusha utakua na mamlaka ya vitu vyote vilipo humo ndani hata ile miziki uliyoipakia
- TUMA MIZIKI KUPITIA GOOGLE DRIVE APP
Fungua Google Drive ukishaishusha kisha Log in kwa kutumia taarifa zako za akaunti yako ya google. Unaweza ukaona mafaili yako yote uliyoyapakia katika google drive.
Chagua file ambalo unapendelea kutuma.ukibonyeza file hilo kuna machaguo mawili yatatokea. Unaweza ukachagua ‘Open In’ au ukabofya kwenye vi doti vitatu kule juu upande wa kulia. Chagua whatsApp katika machagua ya App yatakayotokea alaf chagua rafiki unaetaka mtumia ili kumtumia
Kama Kawaida yetu Teknokona tunakuletea maujanja na mbinu mbali mbali katika vifaa vyako, hii ni kuhusu whatsApp tuambie umeipokea vipi katika sehemu ya comment hapo chini. Usisahau sambaza makala hii tafadhali
Siku Njema!!
No Comment! Be the first one.