fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android Google

Matoleo Ya Android Ya Zamani Kutoweza Ingia Katika Akaunti Ya Google!

Matoleo Ya Android Ya Zamani Kutoweza Ingia Katika Akaunti Ya Google!

Spread the love

Matoleo ya Android 2.3.7  na ya zamani zaidi hayataweza kuingia katika akaunti za google. Hii inamaana kuwa  kama ana kifaa cha Android ambacho kina toleo hilo ….

Au la nyuma zaidi basi haitawezekana kabisa kuingia na akaunti yako ya Google katika kifaa hicho. Android 2.3.7 kwa jina lingine linajulikana kama Gingerbread (tena lile toleo la mwisho la toleo hilo).

Android

Android

Sasa Google wametoa tarehe ambayo itaachana kabisa na matoleo hayo na tarehe hiyo ni septemba 27. Sababu kuu kwao Google wanasema kwamba….

Wanafanya yote hayo ili kuhakikisha kwamba watumaiji wa vifaa ba bidhaa zao wanakuwa salama wakati wanatumia huduma na bidhaa zao.

Baada ya tarehe hiyo unaweza ukawa unaingia katika akaunti hiyo kupitia kifaa chenye toleo la Gingerbread au la zamani zaidi usije ukashangaa unaambiwa nywila yako au taarifa zako hizo sio sahahi.

Simu Za Android

Simu Za Android

Hili sio la kushangaza sana kwani kama una kumbukumbu vizuri ni kwamba toleo la Gingerbread limetokea takribani miaka kumi iliyopita.

SOMA PIA  App 5 Bomba za Muziki kwa Simu Yako ya Android

Vifaa ambavyo vinatumia Android 3.0 (Honeycomb) na kuendelea vitakua salama kabisa maana havitakua na zuizi la aina yeyote.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment hii umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania