Google Drive ilikua inategemewa kwa kiasi kikubwa sana katika kuhakikisha kuwa mtu unahamisha mazungumzo ya WhatsApp kutoka katika kifaa kimoja na kwenda katika kifaa kingine kwa watumiaji wa Android.
Kama inavyojulikana hakuna kitu kibaya kama kutegemea njia moja na ukiangalia njia moja hiyo yenyewe sio kwamba inamilikiwa na WhatsApp – Google Drive iko chini ya kampuni ya Google.
WhatsApp ni moja kati ya mitandao ya kijamii bora kabisa ambayo inatumika kuunganisha dunia nzima kupitia mazungumzo ni sahihi kabisa kwa kampuni hiyo kuja na njia kadha wa kadha ambazo zitahakikisha kuwa wateja wake wanapata kile kilicho bora kabisa.
Njia iliyozoeleka kwa Android ni kwamba mtu lazima ufanye Back Up ya mazungumzo (Chat) zako kwenda katika huduma ya Google Drive na kisha ukiwa na kifaa kingine kipya (au kubadilisha) itakubidi urudishe mazungumzo hayo…
…. Hii ni kupitia na ile Back Up ambayo tayari iko katika mtandao wa Google Drive, cha kujiuliza ni kwamba kwanini mtandao wa WhatsApp haukua na njia yake ya kujitegemea yenyewe?
Kwa sasa kuna kipengele ambacho mtandao wa WhatsApp unakifanyia kazi ambacho kipengele hiki kitawezesha hili bila hata ya kutumia Google Drive.
Chanzo: WABetaInfo.
Kizuri kuhusiana na kipengele hiki ni kwamba kwa kutumia kifaa kimoja unaweza hamisha mazungumzo yako ya WhatsApp kwenda katika kifaa kingine
Cha kufanya ni kwamba lazima uwe umeenda katika eneo la Setting ndani ya mtandao wa WhatsApp na kisha uta-scan QR Code kupitia simu yako mpya ili kuanza zoezi la kuhamisha mazungumzo hayo.
Hapa kidogo kuna watu wameachwa kidogo sio? Fikiria kwa wale ambao vifaa vyao vimeibwa au wamepoteza kwa kuvisahau—hii haiwahusu sio?
Lakini kizuri ni kwamba WhatsApp hawawezi kuishia hapo na pengine wataleta maboresho mazuri kabisa katika njia hii ya kuhamisha mazungumzo (chat).
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je hii umeipokeaje unadhani ni njia sahihi kabisa kwa watumiaji wa Android?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
No Comment! Be the first one.