fbpx

Marufuku kurusha ndege zisizo na rubani/Drones Saudi Arabia

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Saudi Arabia imewatoa wito wanaomiliki ndege zisizokuwa na rubani (Drones) kujisajili na kuomba ruhusa ya kumiliki ndege hizo.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya saa kadhaa baada ya jeshi la Polisi kushambulia ndege isiyokuwa na rubani iliyooruka pembezoni mwa kasri ya mfalme mjini Riyadh usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili.

kurusha ndege

Tukio la kkutumia ndege isiyo na rubani lilipelekea uvumi wa jaribio la mapinduzi na kuyumbisha usalama wa Saudi Arabia.

Hatua hii ya kusajiliwa kwa wamiliki wa ndege hizo kutatoa fursa kwao kuwekewa maeneo ambayo ndege zao zitakuwa zikiruhusiwa kuruka.

Nchi kadhaa duniani zimezuia urukaji holela wa ndege zisizo na rubani ikiwemo Tanzania ambapo kupitia mamlaka ya Usafiri wa Anga, TCAA Julai 11 2017 ilipiga marufuku ndege hizo kuruka bila kibali maalum.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Marufuku matumizi ya Bitcoin nchini Iran
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.