Yapo mambo mengi ambayo yanachangia saana simu yako iwahi kuisha chaji, makala hii inalenga kukusaidia kuyajua mambo muhimu zaid ambayo kwa namna moja ama nyingine yatasaidia kuongeza muda ambao simu yako inakaa na chaji.
Yafuatayo ni mambo ambayo unaweza kuyafanya ili kuongeza muda ambao simu yako inatumia chaji.
-
Punguza mwanga wa simu yako.
Punguza mwanga wa screen ya simu yako mpaka katika kiwango ambacho unakititaji, ama pia unaweza kuset simu yako kuwa kaitka Auto brightness ambapo katika simu za android kupata sehemu hii unaenda katika mpangilio (settings )kisha unachagua display ambayo ukifungua ndani yake basi utakutana sehemu ya kurekebisha mwana wa simu.
2. Zima WiFi kama haitumiki.
Watumiaji wa simu wengi (hasa watumiaji wapya) huwasha WiFi kwa bahati mbaya hii inapelekea simu zao kuisha chaji kwa kasi zaidi ya kawaida. Hakikasha kila wakati ambao hautumii WiFi basi iwe imezimwa katika simu yako maana nayo ni mchango mkubwa katika kumaliza chaji.
settings>WiFi>zima
3. Sitisha huduma zote za location na GPS.
Huduma za location pamoja na GPS ni moja ya huduma ambazo zinatumia saana betri za simu yako, unaweza kwenda kuzima na kusitisha huduma hizi na kuziwasha pindi tu unapozihitaji.
settings> Location > Google Location settings >zima
4. Sitisha “Background Apps”.
Simu janja zote zinauwezo wa kuendesha apps zadi ya moja yaani unaweza kucheza game huku unapokea msg za whats app, app ambayo inaendelea kufanyakazi ingawa wewe umefungua app nyingine inatajwa kuwa ni background app.
Background app sio kitu kizuri ikija kwenye chaji, jinsi unavyokuwa na app nyingi ndivyo unavokuwa unatumia chaji nyingi zaidi.
Ifanye tabia kusitisha app ambazo hauzitumii, kama na wewe ni mvivu kuzima app mara unapomaliza kuzitumia basi jenga tabia ya kuizima na kuiwasha simu yako walau mara nne kwa siku hii itasaidia kuzisitisha app ambazo zilikuwa zinaendeshwa katika background.
5. Ondoa Apps Usizotumia na Tafuta apps mbadala pale panapobidi
Kama tulivyoongelea hapo juu kuna apps nyingi ambazo huwa zinafanya kazi ata pale ambapo uzitumii, saa nyingine ni vigumu kuzifahamu zote na hivyo ushauri bora ni kuwa na tabia ya kupitia apps ulizonazo na kuondoa ambazo hauna ulazima kuwa nazo.
Pia kuna matoleo ya apps maarufu kama vile Facebook na Facebook Messenger ambazo zimepata sifa mbaya sana kwa ulaji wa mkubwa wa kiwango cha chaji katika simu za Android ata pale ambapo huzitumii. Kwa apps kama hizi ni bora utafute apps mbadala, kama vile badala ya app ya Facebook basi unaweza tumia app ya Metal n.k.
6. Zima bluetooth
Bluetooth ni moja ya njia nyepesi za kurusha na kupokea mafaili lakini pia inapowashwa hutumia kiasi kikubwa cha chaji. Hakikisha bluetooth ya simu yako imezimwa kama haitumiki maana nayo huchangia sana kumaliza chaji ya simu.