fbpx
Kompyuta, Maujanja, Windows

Dark Mode kwenye Windows 10, Fahamu jinsi ya kuwezesha. #Windows10 #DarkMode

dark-mode-kwenye-windows-10-fahamu-jinsi-ya-kuwezesha-windows10-darkmode
Sambaza

Leo fahamu jinsi ya kuwezesha dark mode kwenye Windows 10. Muonekano wa giza, yaani Dark Mode, umekuwa maarufu sana siku hizi katika vifaa vya elektroniki kama vile simu na kompyuta.

Microsoft wamewezesha muonekano huo pia kwenye toleo la Windows 10.

Faida za Dark Mode kwenye vifaa vya elektroniki.

  • Inasaidia afya ya macho, mwanga mkali sio mzuri kwa macho yetu
  • Inasaidia kupunguza utumiaji wa chaji kwa asilimia 15 hadi 40 kulingana na app unazotumia
INAYOHUSIANA  Mambo Ya Kuepuka Wakati Wa Kushusha (Download) Mafaili!

Je unataka kuwezesha Dark Mode kwenye kompyuta yako? Fuata hatua hizi;

 

  1. Nenda kwenye menu ya Start, bofya Settings
  2. Ingia kwenye Personalization, upande wa kushoto wa eneo hilo utaona seheme pameandikwa Colors, bofya hapo.
  3. Katika eneo linalofunguka kuna sehemu pameandikwa ‘Choose your default Windows mode/ Choose your color’, bofya na chagua Dark.
dark mode kwenye windows 10
Dark Mode kwenye Windows 10

 

Kwa maujanja mengine zaidi tembelea https://teknolojia.co.tz/teknolojia/maujanja/ , pia usisahau kucomment hapa kuhusu jambo jingine ambalo ungependa kufahamu jinsi ya kufanya kupitia Windows 10.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |