Simu mpya kutoka Samsung amabayo imezinduliwa hivi karibuni imegundulika kuwa ndiyo simu ngumu zaidi kufanyiwa matengenezo katika historia ya simu zillizotengenezwa na kampuni hiyo ya kikorea.
Mtandao maarufu wa iFix ambao umejikita katika kutoa elemu ya jinsi ya kurekebisha simu mbali mbali, uliinyambua simu hiyo mpya ya Samsung Galaxy S7 ili kuifanyia uchambuzi wa kina. Yapo mambo mengi ambayo mtandao huu ulifanikiwa kuyaona katika simu hii ila kwa ujumla ni kwamba waligundua simu hii ndiyo simu ngumu zaidi kufanyiwa matengenezo.
Hii siyo habari nzuri sana kwa watumiaji wa simu hizi hasa ambao ni wakazi wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla kwa kuwa ni wazi watumiaji hupenda kuwa na simu ambayo pindi inapata shida sio ngumu kumpata fundi wa kuirekebisha. Pengine hii ni habari mbaya zaidi kwa mafundi wa simu kwani ni kama kitumbua chao kimeingia mchanga.
Pia watafiti hawa wamegundua kwamba betri ya simu hiyo japokuwa inaweza kutoka bila ya kuhitaji kufungua Motherboard ya simu lakini watengenezaji wameigundisha betri hii kwa kutumia gundi imara na hivyo kuweka ugumu usiokuwa na tija katika kuifungua simu hii.
Uchunguzi huo umebaini kwamba iwapo usb port ya simu hii itaharibika basi utengenezaji wake utahitaji kuondoa kabisa kioo cha simu hii kama sio kukiharibu kabisa.
Zaidi inaelezwa kwamba haiwezekani kabisa kubadilisha kioo cha simu hii bila ya kuharibu display yake (ama kioo cha ndani) kwa maana kwamba iwepo simu yako hii itaharibika kioo basi itabidi ubadilishe mpaka display ya simu yako.
Samsung wanajaribu kubadirika ili kuweza kujidhatiti katika biashara yao ya simu za mikononi, zipo sababu nyingi ambazo zinapelekea simu hii kuwa ngumu kutengeneza; kwanza ni kwa sababu simu hii inakuja na uwezo wa kuzuia maji kuingia ndani na pili simu hii inamtungi wa maji ndani ya simu kwaajiri ya kupooza simu kwa ujumla kinachofanya simu hii ikawa ngumu kufanyia matengenezo ni ubunifu uliotumika kwenye kutengeneza simu yenyewe.
Kama ukimiliki simu hii jambo bora la kufanya pale ikisumbua ni kupeleka kwa watoa huduma rasmi wa Samsung ambapo utakuwa na uhakika zaidi wa usalama dhidi ya uharibifu mkubwa zaidi kwa simu yako. Ugumu wa kufanya marekebisho kwa simu za Samsung ulianza na ujio wa Samsung Galaxy S6 Edge
Kwa mafundi simu wa hapa mjini nadhani mnahitaji kufunga mkanda kiunoni na kukomaa na hawa watengenezaji wa simu kwa kujifunza namna ya kuzifungua na kuzitengeneza, maana ukweli ni kwamba kuna uwezekano watengenezaji wengine wa simu watafuata nyanyo za Samsung.
Chanzo: iFix