fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Magari Tanzania Teknolojia

Huduma ya Usafiri wa Uber Kuja Tanzania, Uganda na Ghana

Huduma ya Usafiri wa Uber Kuja Tanzania, Uganda na Ghana

Spread the love

Huduma ya usafiri ya Uber tayari imeifanya kampuni ya Uber kuwa moja ya kampuni yenye hadhi kubwa na moja inayokuwa kwa kasi zaidi duniani. Baada ya kuwa katika tayari katika miji 7 Afrika  sasa wameona wapo tayari kusambaa zaidi.

Kwa muda sasa wapo katika miji ya nchini Afrika Kusini, Kenya na Nigeria, miji hiyo ilitumika kama eneo la kujifunza hali ya soko kabla ya kusambaa zaidi katika miji mingine ya barani Afrika.

uber

Kwa Kenya huduma hiyo inapatikana katika jiji la Nairobi na tayari njiani kuanza kupatikana katika jiji la Mombasa pia.

SOMA PIA  Vodacom na wizi wa fedha mtandaoni

Changamoto kuu waliyokutana nayo Nairobi na wanayoweza kutana nayo katika jiji la Dar es Salaam ni kupingwa vikali na madereva taxi wanaotoa huduma hiyo tayari. Na ili kuweza kushinda changamoto hii wanajiandaa kuanza kwa kuwavutia watoa huduma hiyo kujiunga na huduma hiyo kwanza ili kuwa wa kwanza katika kunufaika nayo.

Je mfumo wa usafiri wa Uber unafanyaje kazi?

Usafiri wa Uber ni usafiri unaowaunganisha watu wanaoitaji usafiri na madereva taxi, na  ata madereva wa magari spesheli – ya hali ya juu na ya kuvutia.

uber

Nguvu ya huduma ya Uber ni app yake ambayo urahisisha – utafutaji usafiri, malipo n.k

Kupitia app yao utaweza kuwa na akaunti yako, kupata taarifa kuhusu madereva waliokaribu yako, kuita dereva, kuona gharama ya usafiri kupitia app hiyo na ata kulipa kupitia akaunti yako ya benki/Paypal uliyounganisha ndani ya app hiyo na kwa Kenya unaweza kulipa ata kwa kutumia huduma za kibenki za simu (kama vile Mpesa, Airtel Money n.k) kitu ambacho kinaweza kuwezesha kwa Tanzania pia.

SOMA PIA  Utafiti: Watu Wa Miaka 10 - 19 Wanapenda Sana Snapchat Na Instagram!

Bado haijafamika tarehe rasmi ya huduma hiyo kuanza kupatikana ila kwa kiasi kikubwa itakuwa mara baada ya kufanikiwa kuandikisha madereva kadhaa wa taxi na kisha kupata wanaotoa magari mengine yenye hadhi kubwa. Ila huduma hiyo itaanza ndani ya mwaka huu.

SOMA PIA  Teknolojia ya Mabasi Yanayoruhusu Magari mengine kupita chini, Sasa kwenye Skendo ya Utapeli

Endelea kutembelea TeknoKona na tutakupatia taarifa zaidi tukiwa tunafuatilia kwa karibu ujio wa huduma hii.

Vyanzo: AFKInsider na vingine mbalimbali

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. […] Huduma ya usafiri ya UBER ipo njiani kuanza kupatikana Tanzania hivi karibuni. […]

  2. […] Kampuni hiyo ipo njiani kuingia Tanzania. […]

  3. […] kuhusu ujio wa huduma ya usafiri wa Uber Tanzania miezi michache iliyopita. Sasa ni rasmi, huduma ya usafiri ya app ya Uber yaanza rasmi kutoa huduma […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania