fbpx

Magemu ya video yaruhusiwa tena Uchina

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Uchina ni moja ya nchi ambayo haina haiba katika kuweka katazo katika kitu fulani na kwa miezi kadhaa magemu ambayo yanachezwa mtandaoni katika mfumo wa picha jongefu yalikuwa yamekatazwa.

Wapenzi wa michezo hiyo walisubiri kwa zaidi ya miezi kenda ili kuweza kucheza magemu hayo ambapo katika tangazo lake iliweka wazi orodha ya michezo ambayo yaruhusiwa tena baada ya kutokuwepo tangu mwezi Machi 2018.

Je, kwanini michezo hiyo ilizuiliwa?

Magemu ambapo nyuma ya pazia ni uwepo wa teknolojia ambayo kwa wengine ni tishio na ndipo hapo mamlaka husika nchini Uchina ilipoamua kufungia michezo hiyo baada ya watu kuonekana inaleta tishio la watumiaji kutokuwa na fikra pana lakini pia kuleta uraibu!.

yaruhusiwa

Wachina wakifurahia kucheza michezo ya picha za mnato kupitia mtandaoni baada ya katazo lililodumu kwa miezi kadhaa.

Kwa ujumla magemu yapatayo themanini yaruhusiwa tena kurudi kwa wateja wake lakini pia yapo mengine yanaendea kutokuwepo mathalani michezo iliyo chini ya kampuni iitwayo Tencent Holdings LTD.

Vyanzo: Reuters, Engadget

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Hivi Unajua Kama Unaweza Kufanya Haya Na Gmail?
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.