fbpx

Uraibu wa kutumia kompyuta: Serikali ya Korea Kusini yapata suluhisho

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Teknolojia imeleta mambo mengi sana duniani na matumizi ya kompyuta katika shughuli za kila siku kwa ofisi/makampuni mengine ni lazima lakini kuna yale matumizi ambayo ni ya kupindukia.

Nikiuliza leo “Unatumia muda kiasi gani kutumia kompyuta?”, kwa hakika nitapata majibu mengi sana na tofauti tofauti kulingana na kila mtu kompyuta inavyomsaidia kutekeleza kazi zake za kila siku. Serikali ya Korea ya Kusini imetafuta mwarobaini ambao utawafanya wafanyakazi wa serikali kuwa kwenye kompyuta kwa muda uliopangwa tu.

Mpango wa serikali ya Korea Kusini kupunguza matumizi ya muda mrefu ya kompyuta.

Wafanyakazi wanaotumia muda mrefu kuwa kwenye kommpyuta hasa mara baada ya muda rasmi wa kazi wapo katika wakati mgumu kwani serikali ya nchini humo ipo katika mpango wa kuwa wanazima kompyuta mara tu baada ya muda wa kazi.

INAYOHUSIANA  Sasisho jipya la Februari Windows 10 lasababisha matatizo

Wafanyakazi wa nchini humo wanafanya kazi kwa wastani wa saa 2,738 kwa mwaka kulinganisha na wastani wa saa 1,763 kwa mwaka kutoka kwa wafanyakazi wa sekta za umma kwa nchi zingine zilizoendelea.

Uraibu wa kutumia kompyuta

Uraibu wa kutumia kompyuta: Serikali ya nchi hiyo imeona kuzima kompyuta zao itasaidia watu kutofanya kazi katika muda wa ziada na hivyo kupelekea kutokuwa na pesa ya nyongeza kwenye mishahara yao.

Uzimwaji wa kompyuta kwa awamu

Serikali ya Korea Kusini inapanga kuwa itazima kompyuta hizo kwa awamu na awamu ya kwanza intarajiwa kuanza kutekelezwa Machi 30 kila itakapotimu saa 2 usiku. Awamu ya pili itaanza mwezi Aprili kila Ijumaa ya pili na ya nne ya mwezi huo saa 1:30 usiku.

Uraibu wa kutumia kompyuta

Wapo waliosifu mpango huo wa serikali na hatua hiyo itawakumbusha kuwa kuna vitu vingine vya kufanya baada ya saa za kazi.

Awamu ya tatu na ya mwisho itaanza mwezi Mei ambapo kila Ijumaa kompyuta zitakuwa zikizimwa saa 1 usiku. Asilimia 67.1 ya wafanyakazi wameomba wasizimiwe kompyuta zao kulingana na kazi wanazofanya.

Kitu kama hicho sio mara ya kwanza kufanyika kwani wakati fulani serikali ya nchini humo ilikuwa ikizima kompyuta kati ya saa 12 asubuhi na saa sita usiku kuzuia watoto kucheza magemu mtandaoni.

INAYOHUSIANA  HP na kompyuta kwa ajili ya wanafunzi

Serikali za Afrika zikiamua kufanya kitu kama hicho wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali wanaweza wakafurahi/watachukia? 😆  😆  😆

Vyanzo: The Verge, Fortune

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|