fbpx

Mafundi wa vifaa vya kielektroniki kutakiwa kusajiliwa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mafundi wa vifaa vya kielektroniki ambao kiukweli ni wengi karibu kila kona ya Jiji la Dar es Salaam lakini hata katika mikoa mingine wapo wengi tuu sasa imefikiwa wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inataka iwatambue.

Moja kati ya fani ambazo zimekuwa zikionekana zikiajiri watu ambao hawajasoma sana ni mafundi wa vifaa vya kielektroniki (simu, runinga, jokofu, n.k) na kwa sababu hiyo wamekuwa wakikosa weledi/kufuata miiko ya kazi husika.

Lakini pia utakumbuka zaidi ya mwaka mmoja uliopita Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (D. I. T) ilianzisha kozi ya mafundi simu wa ngazi mbalimbali kitu ambacho kwa waliokwenda wakasoma na kupata cheti naamini kuna vitu kadha wa kadha watakuwa wamejiongezea. Hatua nyingine nzuri na muhimu inafuata.

TCRA imewataka mafundi wengi fani hizo (wakiwemo wanaotengeneza kompyuta) kuweza kujisajili kwenye mamlaka hiyo kupitia ofisi za kanda lengo likwa kuwatambua kitu ambacho kitasaidia mambo mengi yanayohusiana na udhibiti.

Mafundi wa vifaa vya kielektroniki

Tanngazo linalohusu mafundi simu kutakiwa kujisajili kwenye mamlaka ya mawasiliano Tanzania.

Zoezi zima la usajili halina gharama zozote (ada) hivyo basi watu wenye fani husika tujitahidi kujisajili ili tutambulike na kuogeza uwaminifu kwa wateja wetu.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTMS)
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.