Makamu Raisi wa kampuni ya Google Inc, Vint Cerf ameonya kwamba, hivi sasa hivi tupo kwenye hatari ya kupoteza kumbukumbu zetu muhimu za kidijitali kutokana na mwenendo wa teknolojia.
Mifumo na teknolojia ya uhifadhi inabadilika kila wakati na anatabiri kuwa kuna kipindi mifumo yote ya sasa itapotea na hivyo itakuwa vigumu kupata kumbukumbu hizi tunazotengeneza sasa.
Akiongea kwenye kongamano la maendeleo ya Sayansi ya Marekani (American Association for the Advancement of Science), Bw. Cerf amekaririwa akisema kwamba, hivi sasa tunatunza picha na video za aina nyingi na hizo zinahitaji programu sahihi za kuzionesha. Mara nyingine, aina hizo hupitwa na wakati na tunabadili aina alafu programu zinahitaji kuonesha hizi aina mpya. Sasa unakuwa unapoteza uhalisi wa ile picha, na baada ya muda picha nzima. Kwa mwenendo huo itakuwa vigumu kwa vizazi vya baadae kujua kuhusu historia yetu.
Makamu wa Raisi huyo, anashauri uvumbuzi wa mfumo utakaotunza teknolojia nzima ya sasa, ili data, mifumo-endeshaji na vifaa vinavyotumika viweze kutumika baadae kuelezea historia ya sasa. Kwa sasa anashauri kila mtu kuchukua hatua na kuchapisha picha na nyaraka muhimu kama njia muhimu ya kujiepusha na upotevu huu unaotokana na mifumo inayopitwa na wakati.
No Comment! Be the first one.