Lenovo ni moja ya kampuni kubwa kabisa katika teknolojia ya kompyuta, kwa mwaka 2014 ilikuwa ikiongoza zaidi sokoni. Na sasa mtandaoni imepata umaarufu si kwa sababu ya kuwa moja ya kampuni kubwa bali ni kwa sababu imegundulika imekuwa ikiuza kompyuta zilizowekwa programu moja inayoenda kinyume na taratibu za kibiashara. Programu hiyo inaitwa SuperFish.
Je SuperFish ni nini?
Hii programu inaingilia mfumo wa mtandao hadi ule ulio salama zaidi yaani HTTPS kwenye vivinjari kama vya Firefox na Chrome kisha inakuletea matangazo mbalimbali kulingana na tabia za utumiaji wa kompyuta yako. Kitu kibaya zaidi ni kutokana na programu hiyo kuwekwa rasmi imekuwa ikitambulika rasmi na mifumo ya usalama ya kompyuta kama vile Windows Firewall, programu za anti-virus kama Windows Defender, Avast n.k. Utambulisho huu unaifanya kuweza kufanya mambo mengi zaidi ya kiusalama na kitu cha ubaya zaidi ni kwamba programu hiyo ya SuperFish inaweza kuathiriwa kiraihisi na ‘hackers’ na wao kutumia programu hiyo kuibia data muhimu kwenye kompyuta husika.
Skendo hii imechafulia jina kampuni hiyo kwa kiasi kikubwa. Lenovo wameomba msamaha kutokana na kitendo chao, makampuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na Microsoft ambao ndio wanawapatia programu endeshaji (OS) ya Windows, yamejitokeza na kuiponda kampuni ya Lenovo kwa kitendo chao.
Inasemekana programu hiyo ya SuperFish iliweza kuingizia kampuni hiyo zaidi ya Tsh bilioni 50 kimapato kwa mwaka jana. (CTV News)
Je unaweza itoaje?
Kwa sasa Microsoft kupitia programu yao ya ‘anti-virus’ ya Windows Defender wamewezesha programu hiyo kuweza kuitambua SuperFish kama programu isiyotakiwa na hivyo itaweza kuitoa kabisa. Pia unaweza kwenda kwenye ‘Control Panel’ -> ‘Uninstall’ na kuiondoa.
Pia kampuni ya Lenovo wameleta programu spesheli kwa ajili ya kuondoa SuperFish, inapatikana kwenye mtandao wao HAPA!
No Comment! Be the first one.