Huko nchini China kwenye mtaa unaoitwa Foreigner Street jijini Chongqing, kumeonekana wazo la kuwarahisishia maisha kama siyo kuwalinda watu wanaotumia simu muda mwingi. Watu kama haoo wamewekewa barabara yao wenyewe kama vile ilivyo kwenye nchi zingine zenye barabara tofauti za waendesha baisikeli na waendao kwa mguu pembeni ya barabara kuu ya magari.
Habari hii imeripotiwa kwenye ukurasa huu wa Kichina, na zaidi kwenye mtandao wa Endgadget amabao unaeleza kwamba jaribio kama hili limewahi kufanyika huko marekani na matokeo yake, ilifahamika kwamba, pamoja na kuweka alama nyingi za upande wa watumia simu barabarani, bado watumiaji hao wa simu hata hawakutambua kwamba kulikuwa na alama zozote kama hizo za kuwaongoza – Ama kweli simu inachukua umakini wa watu! Je, ni muhimu kuwa na barabara kama hii kwenye nchi?
No Comment! Be the first one.