fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Facebook Intaneti

Machapisho ya Kisiasa Facebook kupunguzwa umaarufu wa kufikia watu

Machapisho ya Kisiasa Facebook kupunguzwa umaarufu wa kufikia watu

Machapisho ya kisiasa Facebook yanataanza kuonekana mara chache zaidi kwenye utumiaji wa kawaida wa mtandao huo wa kijamii.

Facebook wamesema wanaanza kufanya majaribio ya teknolojia yao ya kupunguza mara ambazo machapisho/post ya kisiasa yanawafikia watu katika eneo la nyumbani(timeline) la mtandao huo wa kijamii.

Machapisho ya Kisiasa Facebook

Mitandao ya Kijamii inazidi kuchukua sifa ya kuwa vyombo vya habari. Hivi karibuni vimekuwa vikichukua hatua za kuwakataa baadhi ya watu, mfano Bwana Trump kutumia huduma zao. Kwa sasa mitandao hii inaonekana ina nguvu kubwa kuliko ata vyombo vya habari vya kawaida

Majaribio hayo yanaanza kufanyika nchini Kanada, Brazili na Indonesia, ndani ya wiki chache zijazo jambo hilo hilo litawafikia watumiaji wa Facebook wa nchini Marekani.

Tayari Facebook walishaanza kuwaonesha (recommend) watumiaji wake makundi (groups) ya kujiunga yanayojihusisha na maongezi ya kisiasa.

Suala hili linaonekana kuhusishwa mara moja na kuepuka masuala ya kisiasa kuja kuleta madhara mengi kama iliyovyotokea Marekani ambapo mashabiki na wafuasi wa Rais aliyepita Bwana Donald Trump walishambulia bunge la nchi hiyo ili kupinga ushindi wa Rais Biden. Inasemekana mipango ya maandamano na mashambulizi hayo yalifanyika kupitia mitandao ya kijamii, na kwenye Facebook mipango ilihusisha makundi/groups pamoja na kurasa rasmi/Pages.

SOMA PIA  Kim Kardashian Aitetea Application Yake Maarufu!

Mfumo wa kile unachoona unapoingia Facebook/timeline, inahusisha teknolojia mbalimbali za kutambua vitu unapenda na vile ambavyo huwa nashiriki katika mazungumzo navyo.

Kwa kupunguza masuala ya kisiasa kuja kwenye timeline Facebook wanaamini itapunguza watu kujikuta katika mazungumzo ya kisiasa yasiyo na tija.

SOMA PIA  Janga la Ebola: BBC kutoa taarifa kwa WhatsApp

Baada ya majaribio Facebook wanategemea kuleta maboresho hayo kwa watumiaji wake wote. Kwa sasa bado hawajasema hii itakuwa lini.

Ata hivyo Facebook wamesema kurasa rasmi za Serikali na vyombo vya kiserikali havitahusishwa na mabadiliko haya. Vipi una mtazamo gani juu ya maboresho haya?

Vyanzo: Washington Post na vyanzo vingine mbalimbali
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania