fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Apple Apple Watch Teknolojia

Watumiaji wa Apple Watch wafikia milioni 100 duniani kote

Watumiaji wa Apple Watch wafikia milioni 100 duniani kote

tecno

Watumiaji wa Apple Watch wafikia milioni 100 duniani kote, jambo linalofanya Apple Watch kuwa aina ya kifaa cha nne cha Apple kuwa na watumiaji wengi zaidi.

apple watch

Watumiaji wa Apple Watch wazidi kuongezeka duniani kote

Apple Watch ni saa janja kutoka Apple inayotumia programu endeshaji spesheli ya kwa ajili ya kufanya kazi na vifaa vya Apple.

SOMA PIA  Simu Nyembamba Zaidi Kutengenezwa Siku Zijazo

Data zinaonesha kwa kuwa na watumiaji milioni 100, saa ya Apple Watch imekuwa aina ya kifaa cha nne kwa watumiaji wengi zaidi, simu za iPhone zikianza, zikifuatiwa na iPad na kisha kompyuta za Mac.

apple watch

Tutazidi kuona watumiaji wakiongezeka zaidi kwani matoleo mapya yanavyotoka ndivyo matoleo yazamani yanashuka bei na hivyo kuwafikia wengi zaidi

tecno

Hivi karibuni ununuaji na utumiaji wa saa janja umepanda kwa kasi kutokana na kushuka kwa bei ya matoleo ya nyuma, na pia kuja kwa matoleo mapya yenye bei rafiki kwa makundi ya aina mbalimbali. Data za Statistica zinaonesha saa janja za Apple Watch zinashika asimilia 55 ya soko la saa janja/au vifaa vya elektroniki vya kuvaliwa (smart wearables).

SOMA PIA  Utafiti: Hizi ndio Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi katika simu za Android

Hii ni habari njema kwa Apple kwani ina maanisha watumiaji wengi zaidi wa iPhone wanaanza kuona saa za Apple Watch kama moja ya kitu cha kukamilisha pale mtu anapomiliki simu ya Apple. Data zinaonesha pia kufikia mwisho wa mwaka 2022 watumiaji wa saa hizo watawapita watumiaji wa kompyuta za Mac.

Chanzo: 9to5Mac na vingine mbalimbali

SOMA PIA  Fahamu maana na kazi ya CC na BCC kwenye barua pepe
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania