fbpx

Machapisho mubashara kwenye Twitter

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Twitter ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kuboresha mtandao huo wa kijamii sasa wamefanya kitu kingine kwa machapisho mubashara kupitia huko.

Kwa wale ambao tunafuata kurasa kwenye Twitter ambazo mara kwa mara huwa wanapenda kurusha vitu ambavyo vinatokea muda huohuo (mubashara) basi usishangae kuona kurasa hizo ndio za kwanza kabisa kabisakwenye ukurasa wako.

Tafsiri ya kile kilichoboreshwa kwenye Twitter ni mara tu mtu ambae unamfuatilia akarusha matangazo mubashara basi utaweza kuona kile kinachoendelea kuhusu kile kilichochapishwa kwenye uso wa mbele kabisa.

Machapisho mubashara

Mambo ya mubashara yamesogezwa karibu kabisa kwenye Twitter.

Hatua hiyo inalenga kupunguza muda wa kuperuzi huku na kule kwenye Twitter kwa lengo la kutafuta matangazo yanayorushwa muda huohuo na yetote anayetumia Andoid au iOS ataweza kuona mabadiliko hayo.

Vyanzo: Engadget, iPhone in Canada

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Tumia Android Au iOS Kama Mouse Katika Kompyuta!
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.