LinkedIn ni moja ya mitandao ya kijamii ambayo imejikita zaidi katika kukutanisha wataalamu wa mambo mbalimbali na hata kuwa mstari wa mbele katika suala la kuunganisha watu na ajira.
Sababu ya amri hiyo kutolewa kwa makampuni yanayojihusisha na utoaji wa huduma ya intaneti imetokana na kile kilichosemwa kwamba LinkedIn ilikiuka matakwa ya sheria iliyopitishwa miaka miwili iliyopita.
Kila mtandao wa kijamii nchini Urusi unapaswa kutunza taarifa za watumiaji wake katika ‘severs’ zilizopo Urusi na si nje ya Urusi.

Kufungiwa kwa LinkedIn kutaathiri watumiaji wengi nchini humo (Urusi) ambao mpaka sasa una watumiaji karibu mil. 6 na tayari wananchi wa nchini Urusi wameanza kuonyesha kukera na jambo hilo kwa kuandika jumbe mbalimbali kupitia Twitter.
LinkedIn unakuwa ni mtandao wa kwanza kufungiwa kufungiwa kwa mwaka huu ingawa mwaka jana Reddit (mtandao wa kijamii) ulifungiwa kwa mamlaka husika kuamuru makampuni ya simu kuufungia mtandao huo.
Tangu kwa sheria ya kuwa kila kampuni kutuza taarifa za wateja wake katika severs za Urusi makampuni kama Apple na Google wamekuwa wakitimiza sharti hilo; Facebook na Twitter inaaminika kuwa bado hawajaanza kutekeleza matakwa ya sheria hiyo.
Soma pia: Microsoft yainunua LinkedIn.
Katika miaka ya hivi karibuni Urusi imekuwa ikiwabana sana watumiaji wa intaneti jambo ambalo limeongeza udukuzi na kuhatatarisha usalama wa taarifa za watu. Je, unadhani kwa dunia ya sasa kuufungia mtandao fulani utakuwa umetibu tatizo?
Chanzo: Telegraph, mitandao mbalimbali.