Twitter wameendelea kupigana vita ya kubaki katika chati baada ya kuleta QR Code kwa ajiri ya kurahisisha watumiaji wake kuwa-follow watu ama akaunti mbalimbali, huduma hii ililetwa na Snapchat ilipokuja mara ya kwanza na inaonekana imeisaidia sana mtandao huo kusambaa kwa kasi kitu ambacho kimesababisha Twitter na mitandao mingine kuiga.
Ukweli ni kwamba majina yetu katika mitandao ni magumu kidogo kuyatamka ama hata kuandika, hivyo wazo la kwamba unaweza kusambaza picha ambayo mtu akifungua katika simu yake anaweza kuletewa akaunti ya mtumiaji fulani itarahisisha utumiaji wa Twitter, Pengine njia hii itatumiwa zaidi na makampuni na mitandao katika kupata wafuasi wengi zaidi.

Unaipata wapi Code hii katika Twitter!?
Kwa watumiaji wa Twitter wa Android kupata Code hii wanatakiwa kufungua orodha kuu ya upande kushoto ambapo wanaweza ku scan code kwaajiri ya kutafuta akaunti ya mtu mwingine ama unaweza pia kuiona na kusambaza code yako. Kwa watumiaji wa iOS picha ya code hii inapatikana katika orodha kuu ambayo inapatikana katika profile yako.
Baadhi ya wachambuzi wamehoji umuhimu wa QR code wakati tayari watumiaji wa mtandao huu wanaweza kutafuta akaunti mbali mbali kwa kutumia jina mfumo ambao unafanya kazi vizuri tu kwa sasa, tayari Messenger mtandao wa kuchat unaomilikiwa na Facebook umekwisha weka mfumo wa QR lakini haukuwa na mwitikio mkubwa kwa watumiaji.