fbpx
Android, apps, Teknolojia, whatsapp

Namna ya kuwa WhatsApp Tester (Tumia toleo la beta) #Maujanja

namna-ya-kuwa-whatsapp-testermaujanja
Sambaza

Kila pale WhatsApp wanapofanya maboresho (update) ya App yao kwa watumiaji wa kawaida huchukua muda kuwafikia. Au wanapofanya majaribio ya kitu kipya katika App hiyo kwa watumiaji wa kawaida pia huwa ngumu kuwafikia.

Maboresho mapya au majaribio huwa kwa watumiaji wa Iphone tu ambao hutumia Mfumo endeshaji (Oparating system) wa iOS.

Mabadiliko hayo huwa yanaanza kwa watumiaji wa simu za mfumo endeshi wa iOS kwa simu za iPhone na baada ya mwezi mmoja ama zaidi huanza kwa simu za Android.

INAYOHUSIANA  Toleo la Google Play Store linasababisha simu kuisha chaji haraka

Lakini kuna njia ambayo itakufanya mtumiaji wa Android kuwa mtumiaji wa kwanza zaidi kupata Update zote na kwa wakati kama utaifanya.

Na njia yenyewe ni kuwa WhatsApp tester (Mtumiaji wa matoleo ya majaribio ya WhatsApp)

  • Faida yake ni kwamba update zote au majaribio utapata na utaweza kuzitumia kama miongoni mwa watu wa kwanza kama watu wanaotumia mfumo wa iOS.
  • Ukiwa WhatsApp tester utapata update nyingi mapema zaidi ambazo WhatsApp wanakuwa wanazitoa mara kwa mara.
INAYOHUSIANA  WhatsApp yaleta status zenye mtindo wa Snapchat, Facebook waendelea kuiba vizuri!

Njia hii, WhatsApp wameweka ili kupata maoni ya watu kuhusiana na uzuri au ubaya wa Updates zao kabla ya kuwafikia watumiaji wake Dunia nzima.

Fata maelekezo haya ili uwe WhatsApp tester

whatsapp tester whatsapp beta

  1. Ingia Google Search
  2. Kisha andika whatsApp Beta
  3. Fungua ya kwanza kabisa iliyoandikwa WhatsApp beta Tester- Google Play
  4. Utapelekwa katika Page ambayo itakuwa imekuingiza kuwa WhatsApp Tester
  5. Baada ya hapo unaweza kufungua WhatsApp yako na kushuhudia Update zote pindi zikiwekwa na kuweza kuzitumia.
  6. Muhimu angalia kama unahitaji Ku upadate na ufanye hivyo kwa kuingia Google Playstore.

Nini maoni yako kuhusiana na Maujanja hayo ya kuwa WhatsApp tester, au kuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kujaribu na kutumia Update zote za WhatsApp pindi zinapotoka au kufanyiwa majaribio.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.