Utulivu wakati wa kufanya mawasiliano ni kitu muhimu hasa pale inapobidi kusikia yote ambayo yanasemwa na mzungumzaji upande wa pili. Teknolojia ya siku hizi imerahisisha sana suala la “Kuzuia makelele ya nje” na kitu hicho sasa kimefika kwenye Google Meet.
Mara kadhaa tumeshawahi kuandika makala kuhusu Google Meet; moja ya vitu ambavyo inaleta ushindani dhidi ya Zoom, Skype na nyinginezo. Nikuulize unafahamu kuwa unaweza kutumia Google Meet kwenye kompyuta?
Tangu mwezi Juni 2020 kipengele cha kuzuia makelele kwenye Google Meet kwenye kompyuta kinapatikana na hivi karibuni kitaweza kuwepo kwenye Android na iOS.
Nini maana ya kuzuia makekelele ya nje?
HIi ni teknolojia ambayo inaruhusu mtumiaji kuweza kuzuia kutosikia ambacho kinaendelea nje. Mfano unafanya mawasiliano na mtu kwenye Zoom huku ukiwa umeruhusu kipengele hicho maana yake ni kwamba wewe/unayewasiliana nae hataweza kusikia ambayo yanendelea nje ya mazungumzo yenu mathalani ukiwa unaandika/kujibu kitu kwa njia ya maadishi, sauti za wanyama, ndege, magari, n.k.
Jinsi ya kuruhusu kipengele cha kuzuia makelele ya nje kwenye Google Meet kwa kubofya More>>Settings>>Noise cancellation.
Teknolojia hii kwa miaka kadhaa sasa imekuwepo hata kwenye spika za masikioni ambapo mtu anakuwa haweza kusikia kinachoongelewa nje bali kusikia kile tu kinachotoka ndani ya kifaa husika.
Kwa sasa Google imeruhusu kipengele cha kukata sauti za nje kww wanaotumia G-SuiteEnterprise na G-Suite Enterprise for Education kwenye Android/iOS. Je, wewe unatumia Google Meet? Umeipokeaje habari hii?
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
No Comment! Be the first one.