Je unataka kuhifadhi data muda mrefu na bado unajiuliza njia gani ni sahihi zaidi kati ya SSD, HDD au diski za DVD? Hii makala ni kwa ajili ya kukusaidia kukupatia majibu hayo.
Kunaweza kukawa na sababu kadhaa kwa nini unataka kuhakikisha data zako zipo salama kwa muda mrefu wakati hauna matumizi nazo kwa muda huu. Mfano una mafaili ya picha zako za kumbukumbu au ata mafaili mengine ya dokumenti muhimu, bila kujali sababu uliyonayo leo tunakueleza kuhusu njia sahihi za utunzaji wa data hizo.

Soma pia – Fahamu tofauti kati ya diski za HDD na SSD
Kuhifadhi data kwenye disk za SSD kwa muda mrefu
Diski za SSD ni diski za kisasa zaidi katika uhifadhi data, na zikiwa na sifa ya kutoweza kuharibika kwa uharaka. Zina weza kuanguka na bado zikafanya kazi, hii ni sifa tofauti ukilinganisha na diski za HDD. Ingawa diski za SSD zina sifa nyingi bora kuliko za HDD bado kuna sababu diski hizi hazifai kutumika kwa lengo la kuweka data na kuhifadhi sehemu kwa muda mrefu.
Diski za SSD zinategemea sana umeme. Kila diski inavyotumika ndivyo nayo inapata umeme wa kuweza kuutumia katika uhifadhi data ata pale ambapo haijaunganishwa kwenye kompyuta – mfano diski za nje (external disk). Hivyo diski za mfumo wa SSD ni imara kuhifadhi data muda mrefu ila tuu kama diski hiyo itakuwa inachomekwa tena kwenye kompyuta angalau mara 2 hadi 4 kwa mwaka.
Kama unampango wa kuhifadhi data kwenye diski lakini ni data ambazo utapenda kuzitumia kila baada miezi michache basi diski za SSD ni bora zaidi.
Kuhifadhi data kwenye diski za HDD
Ingawa diski za HDD ni za teknolojia ya miaka mingi ukilinganisha na za SDD, bado diski za HDD ni diski bora zaidi kutumia linapokuja suala la uhifadhi wa data kwa muda mrefu. Unachotakiwa kuhakikisha ni kwamba diski inakuwa katika sehemu salama, isiyo na joto kali na nje ya matetemeko au uwezekano wa kudondoshwa. Ukizingatia hayo basi diski za HDD zina uwezo wa kuduma na data kwa muda mrefu bila kupoteza uwezo wa uhifadhi data. Diski hizi haziitaji kuchomekwa kwenye kompyuta mara kwa mara ukilinganisha na diski za SSD ambazo zinatumia teknolojia ya ‘flash diski’ na hivyo zinahitaji umeme kuweza kutopeteza data.
Faida nyingine ya HDD ni uwezo wa kuona dalili za matatizo mapema zaidi. Diski inaweza ikawa inazima alafu kuna muda inafanya kazi vizuri tuu n.k. Ukilinganisha na SSD mambo ni tofauti, diski ya SSD ikifa imekufa.
Diski za SSD
Diski za SSD zinaweza dumu miaka mingi kama zinatumika mara kwa mara, ila kama unataka kuhifadhi data kwa muda mrefu kwenye diski bila kuitumia – ata miaka mitatu, tano na zaidi basi diski za mfumo wa HDD ndio chaguo bora zaidi. Hakikisha tuu ipo sehemu salama dhidi ya joto.
Kama utahifadhi data kwa lengo la muda mrefu katika diski za mfumo wa SSD, basi hakikisha mara kwa mara diski hiyo inachomekwa kwenye kompyuta – ili kuweza kupata umeme. Diski za mfumo wa SSD zinategemea sana umeme katika kuhakikisha zinaendelea kuhifadhi data.
Njia bora zaidi – DVDs spesheli kwa ajili ya utunzaji data wa muda mrefu, Dual Layer DVD/Gold Archival Grade DVD-R
Kuna DVD spesheli kwa ajili ya utunzaji wa data za muda mrefu. Zinaitwa ‘dual layer DVD’, yaani DVD zinazowekwa kitu kingine tena juu ya eneo la data kwa ajili ya kuzilinda dhidi ya ukwanguaji na kuoza.

Kwa mtumiaji wa kawaida tunakushauri utumie diski za mfumo wa HDD kwa utunzaji wa data wa muda mrefu. Mfumo wa dvd za Archival Grade bado hazipatikani kwa watumiaji wa kawaida.
Teknolojia ya diski za mfumo wa teknolojia ya Archival Disc inatengenezwa na kusimamiwa katika makubaliano ya makampuni mawili, Sony na Panasonic. Kwa pamoja wamekubaliana kuhakikisha teknolojia wanazotumia katika utengenezaji na vifaa vya uchomaji (kuweka data kwenye dvd hizo) kuwa moja. Diski za mfumo huu zilianza kupatikana mwaka 2015 sokoni, na ni diski ambazo zina uhakika wa kuhifadhi data kwa miaka 50 na zaidi.
Diski za mfumo wa Archival Disk zinaweza kuhimili maji, joto kali, na vitu vingine vingi ambavyo diski za kawaida haziwezi kuhimili.Kwa sasa diski hizi zina uwezo wa GB 300 hadi TB 1.
No Comment! Be the first one.