fbpx

Jinsi ya kufanya faili kuwa dogo kwenye kompyuta

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Matumizi ya kompyuta yanaweza kuwa makubwa/madogo kulingana na shughuli ambazo zinahitaji kufanikishwa kwa kutumia kifaa hicho ambacho ni msaada kwa watu, makampuni mbalimbali.

Wakati mwingine inatokea kuwa kuna nyaraka nyingi ambazo unatakiwa kuzituma kwa mara moja zimfikie mhusika lakini changamoto inakuwa hufahamu jinsi ya ya kufanikisha hilo hivyo unaishia kuambatanisha moja moja kwenye barua pepe.

Naamini mbinu hii ya kufanya faili kuwa dogo kwenye kompyuta inaweza ikawa inafahamika na watu wengi kupitia programu endeshi Windows 7, Windows 8, n.k lakini ikawa ni changamoto kidogo kufanya kitu hicho kwenye Windows 10.

Kwenye Windows 10 itakubidi ubonyeze kitufe cha upande wa kulia wa kiteuzi (mouse) kisha unachangua send to, menyu ndogo itatokea na bofya kwenye neno “Compressed (zipped) folder“.

faili kuwa dogo

Hatua za kufuata ili kufanya faili kuwa dogo na hatimae kuweza kulituma kwa mara moja.

Kwa yule atayepokea ili kufungua zile nyaraka nyingi alizotumiwa kwa mara moja njia ya rahisi ya kufanya mara baada ya kulipakua kutoka kwenye barua pepe ni kubofya kitufe cha upande wa kulia kwenye kiteuzi (ukiwa umeshabonyeza hilo faili) halafu utachagua neno “Extract to“.

Baada ya hapo utapelekwa sehemu ambapo unataka kulihifadhi faili husika (Local Disk C, D, n.k) na kwa ushauri ni vyema ukachagua kuweka kwenye Local Disk D au kwingineko kulingana na mgawanyiko wa diski uhifadhi kwenye kompyuta lakini si kwenye Local Disk C.

faili kuwa dogo

Unaweza ukalingulia hapohapo kwenye Downloads (Extract here)/ukaamua kwenda kulihifadhi sehemu nyingine.

Ni muhimu kujua namna gani ya kufanikisha vitu vingi kwenye kompyuta bila kutumia mzunguko mrefu na ukweli ni kwamba vipo vitu vingi hiki tulichokielezea ni kimojawapo.

yanzo: LaptopMag, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Microsoft wazuia Sasisho kwenye baadhi ya kompyuta/laptop: Fahamu sababu
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.