Kwa nini ununue ‘WiFi Router’ wakati una teknolojia kubwa inayokuzunguka ambayo inaweza igeuza laptop yako kama kifaa kinachorusha WiFi kwa vifaa vingine kama vile simu na hata laptop nyingine. Kuna baadhi ya vitu unaweza fanya hata wewe mwenyewe na kuepuka kutumia au matumizi mengi ya pesa zako ambazo ungeweza tumia katika mambo mengine.
Leo tutakuelezea jinsi ya kurusha wiFi kwa vifaa vingine kutumia intaneti unayoipata kwenye kompyuta yako (iwe kupitia modem, n.k.
WiFi ni muhimu na inasaidia sana. Kuna baadhi ya ‘Updates’ kwenye simu huwa zinataka fanyika kwa WiFi na sio Vifurushi vya kawaida. Fahamu Namna Ya Kuiwezesha Sasa!
Ni Rahisi sana kuiwezesha kumpyuta yako kufanya hivyi, Fuata maelekezo haya
1. Kwanza kabisa utaihitaji programu ambayo itakuwezesha kurusha WiFi katika laptop yako bure. Zipo nyingi sana ambazo zinaweza kukuwezesha kufanya hilo lakini TeknokonaDotCom inashauri utumie ‘Virtual WiFi Router’
Kuishusha ‘Set up’ Yake Bofya Hapa
2. Ukishaipakua katika kompyuta yako iwezeshe kwa kukubali vigezo na masharti
3. Ukisha maliza yote hayo fungua Virtual WiFi Router kama utavyoona itakuja na ‘User name’ (WiFi Hotspot) na neno siri (123456789) ambazo unaweza kuziona baada ya ku ‘click’ kibox kilichoandikwa ‘Hide’ baada ya hapo unaweza badili jina na neno siri kwa usalama zaidi
Kama inagoma kufunguka na inasema kuna tatizo la .Net Framework v4.0 (au versions nyingine) basi inabidi u install .Net framework kutoka mtandaoni. kufanya hivyo bofya Install .Net Framework.
4. Share Net From
Hii inamaanisha unataka wapi watu waipate Internet unyoisambaza kupitia WiFi Router kutoka kwenye Laptop yako. kama unaonahili linakuchanganya sana unaweza ukaweka tuu ”MTS Internet”.
5. Chagua Namba Za Vifaa Vya Kuvisambazia
Katika Vitual WiFi Router utaona sehemu imeandikwa ‘Set Maximum Peers’ hii inamaanisha namba ya vifaa unazozirushia WiFi. unaweza amua kurusha kwa Kifaa 1 na kuendelea
6. Sasa Ukishamaliza kila kitu hapo bonyeza Start na utakua ushamaliza kila kitu. Hongera! Umeiwezesha Laptop (kompyuta) yako kuweza Kurusha/kusambaza WiFi katika Vifaa Vingine
No Comment! Be the first one.