fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Anga SpaceX

SpaceX na jaribio jingine la Starship, mambo yameharibika kwenye kutua

SpaceX na jaribio jingine la Starship, mambo yameharibika kwenye kutua

tecno

SpaceX na jaribio jingine la Starship, nalo limeenda vizuri hatua zote ila likaenda vibaya tena kwenye kutua. mashabiki wa makubwa yanayofanyika katika sekta ya teknolojia za anga, kama mimi 😀 tarehe 2 Februari wote tulikuwa tunasubiria kwa hamu na kutazama majaribio mengine ya teknolojia za ndege ya Starship.

SpaceX na jaribio jingine

SpaceX na jaribio jingine: Ndege-roketi ya StarShip ilienda vizuri urefu wa kilometa 10 juu ya usawa wa bahari

 

Haya ni majaribio ambayo yashahairishwa mara kadhaa kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi – ila kutokana na hasira za Bwana Elon Musk na vyanzo vingine inaonesha shirika la kusimamia safari za anga la Marekani, FAA, ndio lililosababisha uchelewaji wa majaribio haya kwa siku kadhaa sasa.

SOMA PIA  Mwaka 2017 ulikuwa mwaka salama zaidi kwa safari za anga

Lengo la majaribio

Kupitia SN9 kampuni ya SpaceX inajaribu kupata data za maboresho juu ya utengenezaji wao wa ndege inayotakiwa kuweza kufanikisha safari kati ya dunia yetu na sayari ya Mars, lakini pia ndege hiyo hiyo kuweza kufanikisha safari za duniani kwa miji miwili iliyo mbali ambayo kwa sasa safari zinachukua zaidi masaa matano au nane, na kufanya safari hizo kufanyika chini ya lisaa limoja.

Kupitia Starship, kampuni ya SpaceX itaweza kufanikisha safari za miji ya mbali duniani ndani ya muda mchache, lakini pia ni lengo la SpaceX kutumia teknolojia hii kuwezesha safari za kwenda kutoka duniani kwenda kwenye sayari nyingine.

Majaribio yameenda vibaya, tatizo nini?

SpaceX na jaribio jingine la Starship

SN9 ikiwa inatua, kama unavyoona ilikuwa imechelewa kugeuka. Pembeni yake ni SN10, inategemewa SN10 kufanyiwa majaribio katika kipindi cha miezi hii inayokuja

 

SOMA PIA  Video, Sauti na Picha za Sayari ya Masi / Mirihi katika ubora mkubwa. #NasaPerseverance

Katika majaribio haya, kwa mara nyingine tena ndege hiyo imeshindwa kurudi na kutua salama. Kwa sasa wataalamu wengi walioangalia video ya kutua wanaona kutakuwa na tatizo limefanyika katika kompyuta ya rokeni hiyo – roketi ilishindwa kujiweka kwenye wima unaofaa na pia ikawa imeshashuka chini sana.

Injinia mkuu wa SpaceX Bwana John Insprucker amesema “Kwa mara nyingine, ndege ilikuwa na safari nzuri…. inabidi tuongeze kazi katika kuboresha utuaji”.

Kwa sasa kupitia jaribio hili na la mwezi Disemba tayari inaonekana SpaceX wameshaweza kuifanya SpaceShip kuweza kuruka na kujigeuza angani kwa mafanikio. Kitu pekee cha kuboresha kwa sasa ni utuaji wake tuu.

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania