WhatsApp wamekua wakifanya maboresho mengi sana katika App yao. Wamekuja na hii mpya ambay inajulikana kama ‘Fast Playback’ katika upande wa Voice Note.
Teknolojia hii kazi yake kubwa itakuwa kuweza kuchezesha voice note zako unazozipokea kwenda kwa kasi ambayo utaichagua.
Unaweza kuchagua kasi ya 1x, 1.5x, na hata 2x na huduma hii inapatika kwa WhatsApp ya kwenye vifaa vya Android na iOS pekee.
Play voice messages 1x, 1.5x or even 2x faster. Your choice. Now available on WhatsApp. pic.twitter.com/UW9vRs5py5
— WhatsApp (@WhatsApp) June 3, 2021
Kwa haraka haraka ni kwamba sasisho hili linajikita sana kwenye Voice Note na hutaweza kusikiliza kwa sauti ya kawaida..
Fikiria labda umetumiwa VN ambayo mtu wake anaongea taratibu sana.. unaweza ifanya VN hiyo ikiwa inaenda haraka haraka ili kuokoa muda.
Toleo hili unaweza kulipata kwa kufanya sasisho (update) ya App ya whatsApp katika soko la AppStore au lile la Google PlayStore.

Soma Matoleo Mengine Ya WhatsApp Hapa Na Kila Kitu Kuhusu WhatsApp Hapa
No Comment! Be the first one.