fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps whatsapp

Tegemea Kutumia Akaunti (Moja) Ya WhatsApp Mpaka Kwa Vifaa Vinne!

Tegemea Kutumia Akaunti (Moja) Ya WhatsApp Mpaka Kwa Vifaa Vinne!

Spread the love

Fikiria kama akaunti moja ya whatsApp ikiweza kutumika kwa vifaa mpaka vinne? Ndio ndio hili tulitegemee hivi karibuni kwani mkurugenzi mkuu wa WhatsApp bwana Cathcart, ameliongelea hilo.

Licha ya hivyo hata mmiliki wa kampuni hiyo ya WhatsApp pamoja na ile ya Facebook bwana Mark Zuckerberg aliwaambia WABetaInfo kwamba watumiaji wa App hiyo wakae tayari kwa kipengele hiki.

Toleo hili kama kawaida litaanza kwanza kutolewa ka ‘developers’ ndani ya miezi ya karibuni na kisa baadae ndio toleo litakuwa linapatikana kwa kila mtu.

Licha ya akaunti kuwa imeunganika kwa vifaa vinne kampuni bado inahakikishia watumiaji wake kuwa kipengele chake cha ulinzi na usalama cha ‘end-to-end encryption’ bado kitakua kinafanya kazi kama kawaida.

“Ni changamoto kubwa sana kuweza kuunganisha jumbe za akaunti moja ya WhatsApp kupitia vifaa vinne, lakini tayari tumeshapata ufumbuzi na hili litafanyika hata kama kifaa kimoja kitakua kimekwisha chaji” — Zuckerberg alisema

SOMA PIA  Google Assistant sasa inaweza kujua jina la wimbo unaoimba kwenye simu janja #Masasisho

Vilevile, hawakuishia hapo bali walisema pia watu wajiandae kwa kipengele kipya ambacho kitajulikana kama “view once” ambapo hapa mtu anaweza soma jumbe mara moja tuu na kisha jumbe au taarifa hiyo inafutika.

Kipengele kingine ni “disappearing mode” ambapo hapa ukipawasha basi jumbe zako zote zitaweza kutoweka kila baada zikisomwa.

SOMA PIA  Amazon kuunda programu ya kujipima nguo

kuchati whatsappUkiachana na hayo yote bado WhatsApp haikuweka wazi kuwa ni lini vipengele hivi viwili vitatoka rasmi, lakini kuhusu kutumika kwa vifaa vinne ni miezi ya usoni tuu

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa commnet, hili umelipokeaje? ni hatua nzuri sana kwa WhatsApp sio?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwa Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania