WhatsApp tofauti zinaongeza vionjo vya WhatsApp ya kawaida kwenye simu yako. Unaweza kupata muonekano mzuri zaidi, meseji za kitofauti, kuamua mambo mengi zaidi ya utumiaji na kwa ujumla, kupata ladha tofauti kabisa ya WhatsApp.
Soma hapa kufahamu aina hizi tofauti za WhatsApp na ubora wake – Aina 3 Tofauti za WhatsApp
Kupata ladha tofauti za WhatsApp, unaweza kufanya yafuatayo:
Android:
1. Shusha WhatsApp mbadala hapa:
– WhatsApp Plus
– OGWhatsApp
2. Okoa Meseji zako:
Ni muhimu kufanya ‘back-up’ ya meseji zako. Ingawa WhatsApp inafanya hivi mara kwa mara, ni muhimu kufanya hivi mwenyewe. Ukifanya hivi, utaokoa meseji zako zisipotee unapoweka WhatsApp mpya au hata unapobadili simu.
Kuokoa meseji fanya hivi: Menu-> Settings -> Chat Settings -> Backup conversations.
Subiri kinachoendelea kwenye skrini kiishe.
3. Toa WhatsApp yako ya kawaida:
WhatsApp ya ladha tofauti haiwezi kufanya kazi sambamba na WhatsApp ya kawaida na hivyo, inafaa uitoe (uninstall) kabla ya kuipakia.
Kufanya hivi: Ingia kwenye settings za simu yako -> Application Manager -> tafuta WhatsApp -> Uninstall.
4. Pakia WhatsApp yako mpya na fuata maelekezo ya kawaida ya kuweka WhatsApp.
No Comment! Be the first one.