Hupaswi kufikiria sana pale unaposikia kwa mfano kulipuka kwa betri za simu aina ya Lithium-ion kwani ni jambo ambalo lipo tamati kumalizika.
Tatizo la betri hizo zikiwamo zile zilizoleta shida wakati fulani kwenye Samsung Galaxy Note 7 limesababisha milipuko kadhaa mpaka maamuzi yakatoletewa kusitisha matumizi ya simu hizo na kuondolewa kabisa sokoni.
Hitilafu ya betri za Lithium-ion kulipuka limekuwa moja ya janga kubwa kwa baadhi ya simu tukio ambalo linaweza kusababisha vifo na wengine kupata majeraha kutokana na milipuko huo.
Hasara iliyotokana na kulipuka kwa betri ya Samsung Galaxy Note 7.
Baadhi ya watafiti wamekuja na toleo jipya la betri za Lithium-ion ambazo wanasema kuwa kamwe hazitashika moto kirahisi kwa maana ya kwamba betri hizo zitaendelea kufanya kazi hata kama itakuwa na tatizo kidogo.
Betri za Lithium ndio zinazotumika kwenye simu nyingi. Teknolojia ambayo watafiti wanakuja nayo tayari imeshajaribiwa kwenye betri za ndege zinazoruka zenyewe bila rubani (Drone).
Kuja kwa teknolojia hiyo kutaongeza usalama zaidi wa matumizi ya simu za mkononi na kupunguza hofu kwa watumiaji wake.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.