Hii ndio S Pen ya Samsung Galaxy Note 9

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Wakati Samsung Galaxy Note ya kwanza ilipozinduliwa, ilijumuisha kalamu maalum iitwayo ‘S Pen’ ikiwa na muundo maalum wa kuifanya ihifadhike kirahisi kwa kuichomeka ndani ya simu. Ulikuwa ni ubunifu mpya kabisa wakati huo wa miaka ya 2000.

Lakini kalamu yenyewe (S Pen) ilikuwa rahisi tu. Ndiyo, kwa kiasi fulani ilikuwa na uwezo wa juu kunasa msukumo wa kidole (Touch) hata wa kuigusa kidogo na pia kitufe kidogo kilichowezesha mtumiaji kuiamuru kutekeleza baadhi ya kazi lakini kwa ujumla toleo la kwanza kuingia sokoni ilikuwa ni malighafi ya plastiki tu iliyonakshiwa kiufundi.

Teknolojia ilipofikia kwenye S Pen.

Kalamu mpya ya S Pen iliyozinduliwa kwenye Samsung Galaxy Note 9 ikiwa sehemu ya viambata vya simu himu hiyo ikiwa ni toleo la tisa wa simu hizo imekuwa bora zaidi huku wabunifu wakiwa bado wameendelea kufanya kifaa hicho kubaki na sifa yake ya asili.

S Pen ya Samsung Galaxy Note 9

S Pen inafanya yote ya toleo la la kwanza lakini sifa ya ziada kwenye kifaa hicho ni pamoja na teknolojia ya ‘Bluetooth’ ndani yake.

Mambo 7 ya kwenye kalamu mpya (S PEN) katika Samsung Galaxy Note 9.

Yafuatayo ni mambo saba ya ‘kijanja’ yanayoweza kufanywa na mtumiaji wa S Pen iliyomo katika simu mpya ya Samsung Galaxy Note 9:-

 1. Kuwasha kamera na kupiga Picha. Ina uwezo wa kuiamsha kamera na kupiga picha. Hili huwezekana pale mtumiaji anapobonyeza kitufe kwa kalamu hiyo na kukishikilia kidogo.
 2. Uchukuaji wa picha za ‘Selfie’ kwa urahisi zaidi kwa sababu sasa hutahitajika kushika simu lote mkononi na kidole kuhangaika kupata sehemu ya kubofya ili kupata picha.

  S Pen ya Samsung Galaxy Note 9

  Kinachofanyika sasa, ni kushika simu kwa mkono wowote na kisha picha itapigwa na mkono mwingine wenye S Pen.

 3. Picha kwa juu. Kwa kutumia S Pen mtu anaweza kubadili kirahisi muonekano wa picha wakati tukio zima likichukuliwa kutoka kwa juu. Kwa maana ya kwamba kuweza kupunguza/kuongeza mwaga kabla ya kupiga picha.

 4. Kuongeza/kupunguza sauti. Kwa kutumia kifaa hicho kipya utaweza kurekebisha kirahisi sauti ya muziki na video pindi unaposikiliza ‘Midundo’ au kutazama picha jongefu kutokana na kuwa teknolojia ya bluetooth.

  S Pen ya Samsung Galaxy Note 9

  S Pen ya kwenye Samsung Galaxy Note 9.

 5. Uwasilishaji wa taarifa fupi. Kwa lugha rahisi utaweza kutumia kalamu hiyo kuweza kwenda mbele/kurudi nyuma pale unapokuwa unaeleza kitu kilicho katika mfumo wa maandishi au picha kutoka kwenye simu husika kupitia kifaa fulani (projector).
 6. Inachajiwa kwa sekunde 40 tuu!Kitu hicho kinawezekana kwa sababu betri  yake ni ndogo sana lakini yenye kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu. Chaji yake huisha baada ya kalamu hiyo kutumika walau mara 200. 

  S Pen ya Samsung Galaxy Note 9

  Kimemeshi kinachoweza kuchaji simu (Samsung Galaxy Note 9), saa (Galaxy Watch) na S Pen kwa wakati mmoja.

 7. Kufikia programu tumishi. Jambo lingine ni uwezekano rahisi wa kuiunganisha S Pen na programu tumishi zinazoundwa na watu wengine kwa madhumuni mbalimbali mfano games na video editor.

Kama hiyo haitoshi, kufikia mwisho wa mwaka huu au mwanzoni mwa 2019, S Pen ya Samsung Galaxy Note 9 inatarajiwa kuwa na uwezo wa kufanya kazi nyingine zaidi ili kurahisisha maisha kwa watumiaji wake hususani wale wenye simu hiyo mpya.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Google Waleta 'Plugin' ya Drive kwenye Microsoft Office
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.