fbpx
Samsung, simu, Teknolojia, Uchambuzi

Uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 9 umefanyika

uzinduzi-wa-samsung-galaxy-note-9-umefanyika
Sambaza

Agosti, 9 2018 itabaki kwenye kumbukumbu kwamba ndio siku ambayo Samsung Galaxy Note 9 ilizinduliwa na kumaliza minong’ono ya watu kuhusu sifa ilizonazo simu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kutambulishwa kwa ulimwengu.

Samsung wameweza kuweka tofauti kubwa kati ya toleo lililopita (Samsung Galaxy Note 8) na hili la sasa katika maeneo mbalimbali kama urefu wa kioo, uwezo wa betri, kamera, S-Pen.

Uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 9
Ubora wa kamera kwenye haujabadilika na kubaki MP 12 kwa kamera zote ila tu teknolojia ya kutumia alama ya kidole imewekwa chini kidogo ya kamera ya nyuma.

Mbali tu na kwamba kuna vitu kadha wa kadha ambavyo vimeborwshwa kwenye Samsung Galaxy Note 9 kiujumla ni simu ambayo kwa maneno inaweza kuchukua muda mwinngi kuielezea na hii inatokana na mambo mbalimbali:

Kamera. Kwenye Samsung Galaxy Note 9 kamera yake ina mbwembe nyingi; kile kipengele cha kutambua kitu (AI-Artificial Intelligence) inaweza kutambua vitu takribani 20 (vyakula, wanyama, mimea, n.k) na baada ya hapo kuweza kubadili rangi/mwanga kulingana na eneo husika kabla ya mtu kuamua kupiga picha husika.

INAYOHUSIANA  Youtube: Kipengele cha Dark Mode kwenye simu
Uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 9
Kipengele cha AI kwenye Samsung Galaxy Note 9 ambavyo kinaweza kutambua picha ya kitu hata kama kitu chenyewe hakionekani vizuri.

S-Pen. Safari hii kalamu hii ya kidijiti imeongezewa uwezo kuifanya kuwa na nguvu zaidi zadi; hivi sasa S-Pen ya kwenye Samsung Galaxy Note 9 ina bluetooth na hivyo kuweza kutumika kama kitufe cha kuamuru kupiga picha/kitu kingine chochote ambacho utapenda kuamuru iwapo utabonyeza kitufe hicho kulingana na utakavyopend kuweka kwenye mpangilio (settings).

Uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 9
Hii ndio S-Pen ya kwenye Samsung Galaxy Note 9 ambayo inaweza kufanya mengi zaidi.

Kioo (Muonekano)/Kipuri mama. Hapa simu hii kioo chake kina urefu wa inchi 6.4 na kikiwa ni cha AMOLED Quad HD+. Upande wa kipuri kinachoendesha simu inatumia Snapdragon 845.

RAM/Diski uhifadhi. Upande wa RAM zipo Samsung Galaxy Note 9 aina mbili; moja ina RAM GB 6 na GB 128 memori ya ndani halafu nyingine ina RAM GB 8 na GB 512 diski uhifadhi lakini bado pia unaweza kuweka memori ya ziada ya mpaka TB 1.

INAYOHUSIANA  Samsung ‘wasimamisha' utengenezaji wa Samsung Galaxy Note 7

Betri/Programu endeshi. Kama ambavyo taarifa za fununu zilivyoeleza betri ya kwenye Samsung Galaxy Note 9 ni kweli ina 4000mAh na simu hiyo inakuja na programu endeshi ya Android 8.1.

Uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 9
Rangi ya Samsung Galaxy Note 9+Sen: Kama zinavyoonekana na ndivyo utaikuta kwenye boksi lake.

Mengineyo.

Bado Samsung wameendelea kutoacha kuweka sehemu ya kuchomeka spika za masikioni na onaelezwa programu wezeshi ya DeX imeboreshwa na sasa unaweza kuunganisha simu yako kiurahisi kwenye kioo kikubwa kwa kutumia waya wa HDMI na hivyo kuweza kuitumia kama kompyuta kamili kuunganisha kicharazio na “kipanya“.

Uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 9
Samsung Galaxy Note 9 inakuja katika rangi mbalimbali zikiwemo Bluu, Zambarau, Udhurungi.

Samsung wameruhusu kuanza kuagiza Samsung Galaxy Note 9 kuanzia Agosti, 10 2018 kwa bei ya $999|Tsh. 2,297,7002,875,000(6GBRAM/128GB-Memori ya ndani) na $1,250|Tsh. (8GBRAM/512GB-Diski uhifadhi). Agosti, 24 2018 ndio zitaanza kupatikana kwingineko duniani.

Vyanzo: The Verge, Engadget

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Dondoo kuhusu Samsung Galaxy Note 10 Pro - TeknoKona Teknolojia Tanzania
    May 6, 2019 at 8:16 am

    […] sasa ukenda kwenye maduka ya Samsung  utakutana na simu janja Samsung Galaxy  Note 9 ambayo ilitoka mwezi Agosti 2018. Mwaka huu tayari taarifa mbalimbali zimeshaanza kuenea kuhusu […]