Najua ushawahi kujiuliza ni jinsi gani utaweza kushusha /’download’ vitu mbalimbali kama nyimbo, tamthilia flani unazofuatilia na unapata shida kuziona, makala flani (documentary), au ata filamu flani, vitu ambavyo vanaweza kuchukua muda mrefu kuvi’download kwa kawaida.
Tena ukiangalia suala la mwendo (speed) mdogo wa intaneti hili linakuwa kikwazo, kwani unaweza ukaanza alafu intaneti ikasuambua wakati hata unakaribia kumaliza. Hapa ndo umuhimu wa kutumia mfumo wa ‘torrent’ katika kushusha mafaili makubwa kwa madogo unakuja.
Mfumo huu ni wa umoja katika kushusha kitu, yaani ukianza kushusha faili flani utakuwa unashusha kutoka kwa watu wengi yaani hata maelfu. Fikiria hivi, unandoo na unachota maji, kwa mfumo wa kawaida utakuwa unachota moja kutoka kwenye bomba moja, ila kwa mfumo wa torrent ni sawa na kuchota maji kutoka mabomba mengi kwa wakati mmoja. Hii inasaidia kuongeza mwendo wa intaneti katika kushusha, na faida nyingine ni kwamba ata kama intaneti au umeme utakatika ghafla usihofu kwani baadaye ukija kuwasha faili lijajiendeleza kujishusha pale lilipoishia mara ya mwisho.
Je jinsi gani ya Kutumia?
1. Shusha programu ya BitTorrent:
2. Tambua Sheria
3. Jifunze Misamiati
- Leecher – Mtu anayelishusha(download) ilo faili kwa wakati huo.
- Seeder – Mtu anayepakia(uploading) faili hilo kwa wakati huo. ‘Seeders’ wakiwa wengi, ndio ‘Leechers’ au watu wanaoshusha wataweza kulishusha kwa mwendo mkali zaidi(high speed download).
- Tracker – Sio muhimu sana, ila ni taarifa inayolihusu ‘torrent’ file hilo na usaidia kupata taarifa juu ya Leechers na Seeders la hilo faili kutoka mitandao mbalimbali.
- Faili la Torrent (*.torrent) – Mara nyingi hili ni faili dogo, ukishalishusha huwa linaipa programu yako ya BitTorrent kuhusu wakina nani wanahilo faili (kama filamu, muziki, n.k) ili BitTorrent iweze kulishusha kutoka kwao.
4. Tafuta Mafaili ya Torrent
Kwa kuanzia unaweza kwenda www.kat.ph kwa vitu mbalimbali kama filamu, muziki, tamthilia, programu n.k
This should be so helpful out there, especially for beginners wa haya mambo.
Asante sana Era Barca! Kumbuka kusambaza kwa wengine kupitia ku'share'
Nina ombi moja sasa, fanya makala kuhusu njia rahisi ya/za 'live streaming' (sijui Kiswahili chake kinakuaje hapo)