fbpx
Google, Huawei, Play Store

Huawei Mate 30 Pro kutokuja na apps za Google

huawei-mate-30-pro-kutokuja-na-apps-za-google
Sambaza

Simu janja ya hadhi ya juu ya Huawei Mate 30 Pro inayotegemewa kuja hivi karibuni haitakuja na apps mbalimbali zinazomilikiwa na Google.

Kampuni ya Google imesema uamuzi huo umechangiwa na katazo kutoka serikali ya Marekani kwa makampuni ya nchi hiyo kufanya biashara na kampuni ya Huawei.

huawei mate 30 pro
Muonekano wa simu ya Huawei Mate 30 Pro kulingana na taarifa zilizovuta, simu itatambulishwa rasmi mwezi Septemba

Simu hiyo inategemewa kutambulishwa rasmi mwezi wa tisa na uamuzi huu unaonekana utaathiri mauzo ya simu hiyo katika soko la kimataifa. Tayari simu janja za Huawei zilianza kufanya vizuri sana katika nchi za bara la Ulaya na kutokuwa na apps hizo muhimu wengi wanaamini mauzo ya simu hayo katika bara hilo yatakuwa madogo sana.

INAYOHUSIANA  Huawei waamua kutoa Huawei Mate 20 Lite

Apps za Google kama vile Google Maps, Google PlayStore, Google Search, Kivinjari cha Google, Gmail, na YouTube ni apps muhimu sana kwa watumiaji wengi wa sasa.

google apps google play
Apps za Google zimeshakuwa moja ya sifa muhimu ya kuwa na simu janja hasa katika mataifa yaliyoendelea na mengine mengi nje ya China.

Umuhimu wa apps za Google unaonekana ata kwa watumiaji wa simu za iPhone ambapo apps za Google kama vile YouTube, Maps, Gmail, na Google Photos ni bado maarufu sana ingawa Apple ana huduma za namna hiyo pia.

Kwa nchini Uchina bado simu hiyo itaweza kufanya vizuri kwa kuwa huduma za apps za Google hazipatikani nchini humo kabisa. Na tayari huduma za app ya WeChat ndio huduma zinazoshikilia soko nchini humo na huduma hizo zitaendelea kupatikana kwenye simu zao za nchini humo.

INAYOHUSIANA  Kama unatumia kivinjari cha Google Chrome sasisha kwa usalama

Inasemakana kwa kutoa simu zisizokuja na apps za Google mauzo ya simu za Huawei yataporomoka kwa asilimia 40 hadi 60 (kulingana na jarida la Bloomberg). Tayari uongozi wa Huawei umesema suala hilo linaweza sababisha wao kupoteza mapato ya dola bilioni 10 kwa mwaka.

Je kwa mtazamo wako utaweza kutumia au kununua simu janja inayokuja bila ya apps za Google?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |