fbpx

Huawei yakiri kutoipita Samsung kwa mauzo ya simu mwaka huu

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Huawei yakiri kutoipita Samsung mwaka huu. Lengo la kampuni ya Huawei la kuipiku Samsung kwa mwaka huu na kuwa namba moja duniani kwa mauzo ya simu, limeonekana kuingia dosari baada ya kuwekewa vikwazo na serikali ya Marekani.

Huawei yakiri kutoipita Samsung kimauzo

Katika kipindi hichi cha miaka miwili – mitatu kampuni ya Huawei imejitahidi kuongeza ubora kwenye simu inazozileta na hadi kuanza kupata umaarufu na kupokelewa vizuri kwenye soko la Ulaya na hasa hasa kwenye sifa za simu za bei ya juu – eneo ambalo Samsung ilitawala kwa kipindi kirefu

Uongozi wa Huawei umekubali sasa itachukua muda mrefu kuliko ilivyo tarajiwa kuja kuipiku Samsung kutoka namba moja katika mauzo ya simu.

INAYOHUSIANA  Hii ndio simu ya kwanza ya mkononi kutengenezwa na Samsung!

Akizungumza Afisa wa kimkakati wa Consumer Business Group, Bwana Shao Yang alisema itakuwa ngumu kwa Huawei kuipiku Samsung katika robo ya nne ya 2019 kufuatia zuio la biashara ndani ya marekani.

mauzo ya simu mwaka 2019

Huawei yakiri kutoipita Samsung: Ripoti ya robo ya kwanza ya mwaka 2019 (iliyoishia Machi 2019) ilionesha Huawei wakiwa namba mbili, namba tatu ikichukuliwa na Apple huku Xiaomi wakishika namba nne.

Alisema Huawei imeuza simu takribani 500,000 hadi 600,000 kwa mwanzoni mwa mwaka, na ilitarajiwa kuuza simu kati ya 101 milioni hadi 121 mwishoni mwa mwaka huu.

INAYOHUSIANA  Simu ya Infinix Hot 6 pro imekuja na prosesa ya Snapdragon

Lakini kufuatia kuzuiwa kuuza simu zake ndani ya Marekani na zuio la kutotumia kwa huduma za Google kama Play Store kumeathiri na kutaathiri kwa kiasi kikubwa soko la simu hizo hususani nje ya soko la China na hasa hasa ikiwa barani Ulaya.

Kampuni ya Samsung ambayo ndio inayoongoza kwa uuzaji wa simu nyingi Duniani, inafaidika na majanga haya yaliyoikumba Huawei hivyo kuendelea kujikita kileleni kwa mauzo ya simu duniani.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.