fbpx

Tetesi: Toleo la Android la Huawei lina kasi ya 60% zaidi ya toleo la Google

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Chombo cha habari cha China cha Global Times kimerepoti ya kwamba toleo la Android la Huawei lina kasi ya asilimia 60 zaidi ukilinganisha na toleo la Android kutoka Google.

Watafiti wengi wameshasema ya kwamba katika katazo la serikali ya Marekani kwa makampuni ya nchini humo kufanya kazi na Huawei litaathiri sana eneo la mahusiano ya Huawei na kampuni ya Google.

Haraka haraka wengi waliona ni Huawei atakayeathirika zaidi, ila baada ya muda wengi wamekubali ya kwamba wote wawili wataathirika, huku mauzo ya Huawei yakiporomoka katika mataifa ya Ulaya na pia huku Google akikosa biashara kubwa inayotegemea toleo lake la Android linalokuja na PlayStore.

INAYOHUSIANA  Uchambuzi : Ifahamu Tecno Boom J7, Bei na Uwezo Wake!

Toleo la Android la Huawei

Toleo la programu endeshaji la Android kutoka Huawei linalokwenda kwa jina Hongmeng OS (Ark OS nje ya China) lipo kwenye matengenezo na maboresho ambapo inasemekana tayari Huawei amewapatia pia makampuni mengine kama vile Xiaomi na Tencent (watengenezaji wa Tecno) kwa ajili ya majaribio.

Tayari Huawei imeomba hakimiliki ya jina la Hongmeng OS kwenye mataifa mbalimbali duniani.

Taarifa hizi hazijapata uthibitisho mkubwa wa zaidi ya habari iliyotolewa na chombo cha habari cha GlobalTimes na kunakiliwa na vyombo vingine vya kimataifa. Kuna watafiti ambao pia wanahisi hii inaweza ikawa ni vita ya kihabari zaidi (PR), inaweza ikawa imelipiwa kuzidi kuionesha marekani ya kwamba Huawei ipo vizuri kusogea mbele bila kutegemea toleo la Android kutoka Google.

INAYOHUSIANA  Kutopatikana kwa Google Allo

Google wachukua hatua kuitetea Huawei nchini Marekani;

Tayari Google wameadhisha mkakati mkubwa wa kujaribu kubadilisha mtazamo wa serikali na vyombo vyao vya kiusalama ili katazo lilitolewa na serikali hiyo libadilishwe. Google wamekuwa wakisema uamuzi huu wa serikali ya Marekani ndio utazidi kuchangia kutokuwa kwa usalama kwa watumiaji mamilioni wanaotumia au watakaotumia vifaa vya Huawei.

Kwani wanaamini wao kama Google huwa wanawahi kuona matatizo ya kiusalama ya ndani ya Android mapema zaidi na katazo hili litawaweka watu mbalimbali kwenye hatari ya udukuzi, hii ikiwa ni pamoja na watu kwenye serikali ya Marekani wataowatumia watumiaji wa Huawei data muhimu bila wao kufahamu simu ya mpokeaji.

INAYOHUSIANA  LG watoa simu janja mpya mwezi Mei 2018

Vita hii inaendelea, Teknokona tutaendelea kukupa taarifa zaidi. Je unadhani Marekani atalegeza na kuondoa pingamizi hili?

Vyanzo: GlobalTimes na vyanzo vingine
Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |