fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Google Mtandao wa Kijamii Teknolojia YouTube

Google Yamlipa Hacker Wa Urusi Kwa Kugundua Dosari Youtube!

Google Yamlipa Hacker Wa Urusi Kwa Kugundua Dosari Youtube!

Spread the love

youtuubeGoogle wamemlipa dola za kimarekani 5000 kwa hacker wa urusi kwa kugundua mapungufu ya youtube. Mitandao mingi mikubwa kama vile facebook huwa ina desturi ya kutoa zawadi kwa wataalamu wa kumpyuta endapo watagundua dosari flani katika mitandao hiyo.

Jamaa (Mrusi) aligundua njia ya kufuta video youtube kwa sekunde chache tuu. Jamaa huyo wa miaka 21, Kamil Hismatullin katika makala moja alielezea jinsi anavyoweza kufuta video hizo. Alisema anaponakili sehemu ya anuani ya video hiyo hivyo ana uwezo wa kuifuta ndani ya nusu dakika.

SOMA PIA  Miaka minne ya masasisho ya programu endeshi kwenye simu janja za Samsung

“Kwa ujumla nimetumia masaa 6 hadi 7 nikifanya tafiti. Pia nimepigana vikali na haja yangu (Matamanio) ya kutaka kufuta video zote za Bieber (Justin Bieber)”- Hismatullin, aliandika hivyo kuelezea matamanio yake ya kutaka kufuta video za msanii huyo.

Kwa  kutoka kwa bwana Hismatullin anasema kuwa dosari hiyo inaweza tokea kweli na kusababisha majanga makubwa sana kama vile kufuta video za mtu, kutoa taarifa zisizo na uhakika kwa watu hata na kisumbua youtube kama kampuni katika kipindi cha mda mchache.

SOMA PIA  Undani wa kina kuhusu Asus Zenfone 8 Flip

Licha ya kuchukulia hiyo kama fursa ya kufanya mambo yake mengine  (Kama vile kufuta video za Bieber,  Ha!). Aliamua kuripoti mapungufu hayo katika uongozi wa youtube.

Hismatullin aliripoti tatizo hilo katika uongozi wa Google mapema asubuhi ya tarehe 4 mwezi aprili jijini San Francisco. Na kuongezea kuwa allishangazwa na majibu ya haraka kutoka katika kamati ya ulinzi na usalama ya Google. Dosari hiyo ilifanyiwa kazi na baada ya masaa tuu mambo yakawa shwari na akapata dola za kimarekani 5000 kama zawadi

SOMA PIA  Twitter Yafanya Makosa: Akaunti Mbalimbali Kuwa 'Verified Kimakosa!

Kutokana na Bw. Hismatullin aligundua dosari hiyo pale alipokua akiifanyia vipimo YouTube Creator Studio, Huduma ambayo inawaruhusu watu kuangalia taarifa za huduma za video zao pale wanapozipandisha youtube kupitia App.

Kusoma Zaidi Ingia Mtandao Wa BBC

Kama wewe ni mtaalamu kwa mambo haya kaa bize na kompyuta yako na wewe unaweza ukaondoka na madola kadhaaaaaa..

Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania