Google wamethibitisha kwamba wanafanyia majaribio utaratibu wa watu kutumia akaunti zao bila ya kuingiza password (nywila), hatua hii itawafanya watumiaji wa akaunti za Google kutumia simu zao kuingia katika akaunti zao.
Kinachofanyika ni kwamba kila mtumiaji atakapo kuwa anataka kuingia katika akaunti yake basi google watamtumia notification katika simu yake na atakapokubali ujumbe huu ataruhusiwa kuingia katika akaunti yake.
Msemaji wa Google amesema kwamba wamewaalika watumiaji wachache kujaribu njia mpya ya kuingia katika akaunti zao kwa kutumia simu zao, na kuendelea kudai kwamba siku za kuendelea kukariri password zinahesabika.
Huduma hii inafanyiwa majaribio kwa watumiaji wa Os za Android na iOS, waliobahatika kualikwa kuijaribu huduma hiyo wanasema kwamba ili kutumia unahitaji ku set simu yako kwanza na baada ya kufanya hivyo kila utakapo taka kuingia katika akaunti yako kutoka katika kompyuta nyingine basi utatakiwa kufungua simu yako na kukubali notification uliyotumiwa.
Hii huduma inawafaa watu ambao ni wasahaulifu ambao hawawezi kukumbuka password ngumu hivyo wanaamua kutengeneza password nyepesi. Hata hivyo wakati wowote unaweza kurudi kutumia njia ya password muda wowote kama hutaweza kutumia simu.
Google ni kampuni ambayo imejijengea sifa kubwa katika kuhakikisha kwamba wateja wake wanakuwa salama kila wakati, hatua hii ni kuhakikisha kwamba watumiaji wote wanakuwa na nywila ngumu hata kama hawana kumbukumbu nzuri.
Picha zilizotumika hapa zimechapishwa na jarida la GSM ARENA
No Comment! Be the first one.