fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Google Google Pixels simu Smartphones

Google Waachana Na Tundu La ‘EarPhone’ Kuanzia Toleo La Pixel 6A!

Google Waachana Na Tundu La ‘EarPhone’ Kuanzia Toleo La Pixel 6A!

Spread the love

Google Pixel ni simu janja nzuri sana na zinasifika sana katika katika swala zima la picha na hata utendaji wake wa kazi.

Google kupitia simu yao mpya inayokwenda kwa jina la Google Pixel 6A, ambayo wameitangaza hivi karibuni, inakuja na vipengele vingi lakini sio tundu la spika za masikio.

Pixel 6A

Pixel 6A

Hii kwa maana nyingine Google kupitia simu hiyo wanajiunga katika chama cha simu zingine ambazo zilaiachana kabisa na tundu hilo mfano mzuri ni simu za iPhone.

Lakini hii haimaanishi kwamba matoleo mengine ya Pixel yatakuwa hayana tundu hilo, lakini pia haimaanishi kama hayatakua nalo —umeelewa hahaha?

Kumbuka pia kampuni ya Google ina spika za masikio ambazo hazina nyaya (Wireless) pengine ndio watakua wanatumia kigezo hiki ili kuweza kuuza bidhaa hiyo.

Bei ya Pixel 6A

Bei ya Pixel 6A

Kwa sasa matoleo ya simu ya Pixel kutoka Google yanafanya vizuri sana katika soko, tuone na toleo hili litafanya vipi katika soko.

SOMA PIA  Sifa za Undani - Simu ya Tecno Phantom 6 Plus

Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment maono yako ni yapi katika swala hili zima la kutoa tundu la spika za masikio katika simu janja?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

SOMA PIA  WhatsApp kupambana na taarifa za uongo

Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania