fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Google Kuhamasisha Utumiaji Wa Umeme wa Jua

Google Kuhamasisha Utumiaji Wa Umeme wa Jua

Spread the love

Kampuni ya Google Imefungua kurasa mpya katika huduma zake na teknolojia kwa ujumla baada kuanzisha huduma ya kuhamasisha Utumiaji wa umeme wa jua, huduma hiyo ambayo inapigiwa upatu na wanamazingira hasa kwa kuwa itaongeza watumiaji wa umeme huu wa jua ambao ni rafiki wa mazingira.

google-tanzania

Mradi huo uliopewa jina la “Google sunroof project” Unatumia taarifa za Google ili kuweza kuwasaidia wateja wake kujua kiasi kinacho hitajika kuunganisha umeme wa jua, kujua ni shilingi ngapi utaokoa pindi utakapo funga umeme wa jua na kiasi gani cha jua paa lako linapata kwa siku. Mradi huu ambao kwa sasa utaanza kwa sehemu za San Fransisco huko Marekani lakini baadae utasambaa pengine dunia nzima.

SOMA PIA  Zijue Laptop Zinazoendeshwa Na 'Google Chrome OS' Maarufu Kama Chromebook!

project-sunroof-970-80

Kwa kutumia picha za satelite pamoja na taarifa za kwenye database zake mbali mbali, Google wataweza kukadiria gharama za kufunga vifaa vya sola katika nyumba yako wewe, pia wataweza kukadiria kwa mwaka ni kiasi gani cha jua kitatua katika paa la nyumba yako na utakacho hitaji ni kuingiza tu anuani ya mahali nyumba yako ilipo. Pia watakushauri juu ya makampuni ambayo yanafanya shughuri za kufunga umeme wa jua kwa maeneo ya karibu na nyumba yako.

prjtsnunrp8u

Hii ni hatua kubwa kwa kampuni ya Google ambayo kama ilivyo kwa wapinzani wake imekuwa ikijitahidi kuwafikia watumiaji wengi zaidi kwa kuleta teknolojia mbalimbali za kitofauti na zenye msaada kwa watu katika hali mbalimbali.

Soma Pia – ALPHABET: Kampuni ya Google Yafanyiwa Mabadiliko Makubwa, Yagawanywa!

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania